Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 15:50

Majeshi ya Somalia yauwa darzeni ya magaidi wa al-Shabab


FILE - Wanawake wakipita katika nyumba na gari yaliyoharibiwa kabisa na mlipuko uliofanywa na wapiganaji wa al-Shabab mjini Mogadishu, Somalia, Feb. 16, 2022.
FILE - Wanawake wakipita katika nyumba na gari yaliyoharibiwa kabisa na mlipuko uliofanywa na wapiganaji wa al-Shabab mjini Mogadishu, Somalia, Feb. 16, 2022.

Darzeni ya watu wameuawa katika mapigano makali kati ya wakazi wanaosaidiwa na majeshi ya serikali ya Somalia na wanamgambo wa al-Shabaab katika mji wa Adado katikati ya Somalia, mashahidi na maafisa wa kieneo wameiambia VOA Ijumaa.

Walioshuhudia tukio hilo na maafisa wa Somalia katika mkoa huo walisema mapigano yalianza wakati wanachama wa kikundi cha kigaidi kilipovamia mji mdogo wa Bahdo, takriban kilomita 60 mashariki mwa Adado.

Msemaji wa Jeshi la Somalia Yabal Haji Aden aliiambia VOA kuwa wanamgambo hao walianza kushambulia kwa kutumia gari la kujitoa mhanga lililokuwa na vilipuzi, lililipuka karibu na eneo la kuingia mjini humo. Na hapo ndipo mapigano makali ya mtaani yalipoanza kati ya wapiganaji wa al-Shabab na wanamgambo wa eneo la mji huo, ambao walisaidiwa na vikosi vya jeshi la Somalia.

“Walijaribu kulipua magari matatu yaliyokuwa yamebeba vilipuzi … moja wapo [ambalo] lililipuka wanajeshi wetu walipolipiga na gruneti lililorushwa na roketi,” alisema msemaji huyo. “Baadae walilitelekeza gari la pili na gari la tatu lilifanikiwa kukimbia.”

Gavana wa mkoa wa Galguduud Ali Elmi Ganey alisema majeshi ya ushirika yaliwauwa takriban wapiganaji 47 kutoka katika kikundi chenye misimamo mikali.

“Magaidi hawa wameonja umauti, ndani na nje ya mji huo. Waliacha miili ya watu wao 47, bunduki na silaha nyingine,” alisema.

Wakazi wa mji huo na maafisa kadhaa walisema watoto watatu, kiongozi maarufu wa kidini na wanajeshi watatu waliuawa wakati wa mapigano hayo.

Bahdo inajulikana kuwa ni kituo cha wanazuoni wa Kiislam waadilifu, gavana alisema, akieleza kuwa wapiganaji wafuasi wa kikundi cha wanamgambo wa Sufi Islamist wasio na misimamo mikali maarufu kama Ahlu-Sunna Wal- Jamaa—kikundi chenye uhusiano na Jeshi la Somalia wakiiona al-Shabab wenye msimamo mkali kama maadui – walishiriki katika mapigano hayo.

Kikundi cha Ahlu-Sunna Wal-Jamaa kilianzisha vita dhidi ya wanamgambo wa al-Shabab mwishoni mwa mwaka 2008 kutokana na tofauti za kimadhehebu lakini pia kimewahi kupambana na majeshi ya serikali kutokana na tofauti za kisiasa na udhibiti wa katikati ya mji wa Somalia.

XS
SM
MD
LG