Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 13:06

Umoja wa Afrika waadhimisha miaka 59


Mwenyekiti wa sasa wa AU, ambaye pia ni rais wa Senegal Macky Sall
Mwenyekiti wa sasa wa AU, ambaye pia ni rais wa Senegal Macky Sall

Viongozi wa nchi za Africa wanakutana mjini Malabo, Equatorial Guinea kwa mkutano wa siku tatu kuzungumzia masuala la lishe bora na usalama wa chakula.

Mkutano huo unafanyika katika kuadhimisha Mei 25 ambayo ni siku ya Afrika inayoadhimisha kutiwa saini kuanzishwa kwa Umoja wa nchi za Afrika OAU, ambayo nafasi yake ilichukuliwa miaka 20 iliyopita na Umoja wa wa Afrika AU.

Mkutano huo unaongozwa na mwenyekiti wa sasa wa AU,Rais wa Senegal Macky Sall utazingatia kwanza suala la afya, mabadiliko ya hali ya hewa na mzozo wa upungufu wa chakula barani humo.

Kwa upande mwengine Umoja wa Matiafa umetoa ripoti wiki hii kueleza kwamba karibu watu milioni 200 wanakabiliwa na hatari ya nja barani Afrika na mashariki ya kati kutokana na vita vya Ukraine, na hasa hali ya ukame huko pembe mwa Afrika.

Mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya Umoja wa Mataifa Achim Steiner akizungumza kwenye mkutano wa uchumi duniani huko Davos ameonya kwamba mamilioni ya waafrika watashindwa kumudu kununua chakula kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu.

Siku ya Jumamosi, viongozi hao watazungumzia kuhusu vita dhidi ya ugaidi, hasa kwenye kanda ya Sahel, Msimbiji na Somalia pamoja na mapinduzi ya serikali yaliyofanyika katika baadhi ya mataifa ya Afrika magharibi miaka miwili iliyopita.
Wakati viongozi hao wakikutana Malabo,ofisi ya wajumbe wa vijana kwenye AU imesema kwamba inalenga kuwarai vijana ndani na nje ya Afrika kushiriki katika kuleta maendeleo endelevu wakati pia wakibuni mazungumzo baina ya vizazi tofauti. Tangu wakati huo waafrika kutoka kila sehemu wmekuwa wakipanga hafla za kusherehekea maisha ya watu wa Afrika.

XS
SM
MD
LG