Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 12:49

Rais Mpya wa Somalia amemteua Hamza Barre kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo


Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud (L) akipeana mkono na Waziri Mkuu mteule Hamza Abdi Barre

Rais mpya wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, amemteua mbunge kutoka baraza kuu la bunge Hamza Abdi Barre kuwa Waziri Mkuu mpya.

Mohamud alitoa tangazo hilo kwenye makazi ya Rais siku ya Jumatano. “Nimezingatia uamuzi wangu baada ya kutathmini ufahamu, uzoefu, pamoja na uwezo wa Hamza, kisha nikafikia hitimisho kwamba yeye ndio mtu sahihi, ambaye anaweza kutekeleza jukumu hili jipya katika Somalia hii mpya kwa wakati huu mpya” alisema.

Aliwataka wabunge kumwidhinisha Waziri Mkuu mpya haraka na kusema amemtaka Barre kuendeleza vipaumbele muhimu vya serikali mpya ikiwa ni pamoja na usalama, kukabiliana na ukame, maridhiano, maendeleo ya jamii na kukabiliana na majanga ya hali ya hewa.

XS
SM
MD
LG