Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:14

Majeshi ya Somalia yakamata mji mpya


Majeshi ya AU yakifanya doria na kifaru katika mji wa mogadishu
Majeshi ya AU yakifanya doria na kifaru katika mji wa mogadishu

Majeshi yanayounga mkono serikali ya Somalia yamechukua udhibiti wa eneo lilikuwa likidhibitiwa na wanamgambo wa al- Shabab katika mji mkuu wa Mogadishu.

Msemaji wa walinda amani wa umoja wa afrika- AU huko Somalia meja Paddy Ankunda amesema majeshi ya umoja wa afrika yalikamata eneo hilo katika shambulizi alhamisi iliyopita.

Maafisa wa somalia wanasema mashambulizi dhidi ya al- shabab hivi sasa yamehamia karibu na soko la Bakara eneo ambalo ni ngome ya waasi.

Maafisa wa usalama wanalaumu wanamgambo wenye uhusiano na al- Qaida kufanya shambulizi la bomu katika mji wa Mogadishu jumatatu ambalo limeuwa wanajeshi wanne wanaoiunga mkono serikali.

Maafisa wanaamini kuwa al-shabab walitega bomu ardhini ambalo lililipuka katika msikiti ambako wanajeshi wanakutana mara kwa mara.

Serikali ya Somalia na majeshi ya umoja wa mataifa yamepata udhibiti mdogo lakini ulio imara dhidi ya wanamgambo wa al- Shabab tangu walipoanzisha shambulizi mwezi februari.

Kundi hilo la waislamu wenye msimamo mkali limedhibiti eneo kubwa la Mogadishu na sehemu kubwa ya kusini na katikati ya Somalia tangu mwaka 2008.

Al –Shabab inajaribu kuipindua serikali inayoungwa mkono na umoja wa mataifa ili iweze kuweka serikali ya kiislamu itakayokuwa na sheria kali za kiislamu za sharia.

XS
SM
MD
LG