Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:07

Polisi waua majambazi wanne Dar es Salaam


Simon Sirro
Simon Sirro

Majambazi wenye silaha za moto saa mbili usiku Ijumaa walivamia katika eneo la Kariakoo wakitaka kupora fedha katika maduka yaliyopo kwenye mtaa wa Aggrey na Livingstone.

Kwa upande wao Polisi walifanikiwa kuwaua majambazi hao katika tukio hilo.

Zacharia Sijaha ambaye ni shuhuda na miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika tukio hilo alisema muda mfupi baada ya majambazi hao kuvamia na kupiga risasi hewani polisi walijibu mapigo hayo na kuweza kuwaua wote wanne.

“Nilikuwa kwenye biashara ya chipsi nje ya duka, ghafla nikaowaona watu wakishuka kwenye pikipiki na muda huo huo wakapiga risasi na kutuamuru tulale. Bahati kumbe polisi nao walikuwepo nao wakajibu risasi hizo na kuwashambulia majambazi hao,”

"Nikiwa chini nimepigwa taharuki risasi ziliendelea kurindima ghafla moja ikawa imenipata mguuni," alisema.

Ameongeza kuwa Polisi walimchukua wakampeleka Muhimbili lakini baada ya kufanyiwa vipimo ikaonekana hajaathirika kwenye mfupa.

Baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la polisi Dar es Salaam kwa kuweza kuwadhibiti majambazi hao mara moja.

XS
SM
MD
LG