Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 14:43

Majaji maarufu wa Afrika wawasili Kenya kufuatilia kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi


Dr Willian Ruto (kushoto) na Bw Raila Odinga
Dr Willian Ruto (kushoto) na Bw Raila Odinga

Jopo la Majaji Maarufu wa Afrika limewasili nchini Kenya kufuatilia kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Urais  Kenya 2022, ambapo kongamano linafanyika kabla ya kesi kuanza kusikilizwa Jumanne.

Kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na mgombea urais Raila Odinga, kati ya wagombea wanane wengine, anapinga matokeo ya upigaji kura wa Agosti 9 ambapo Makamu Rais William Ruto alitangazwa Rais mteule kwa kupata asilima 50.49 ya kura.

Dkt Ruto alitangazwa mshindi huku makamishna wanne wa tume ya uchaguzi IEBC, walimshutumu mwenyekiti Wafula Chebukati kwa kuuteka mchakato huo na kufanya maamuzi ya kumtangaza mshindi peke yake.

Jopo la wanachama wa Safu ya Majaji wa Afrika (AJJF) linaongozwa na Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.

Majaji wengine ni Lillian Tibatemwa -Ekirikubinza wa Mahakama ya Juu ya Uganda, Ivy Kamanga kutoka Mahakama ya Juu ya Rufaa ya Malawi, Moses Chinhengo kutoka Mahakama ya Rufaa, Lesotho, na Henry Boissie Mbha, Rais wa Mahakama ya Uchaguzi ya Afrika Kusini.

Jopo hilo litahudhuria vikao vyote vya Mahakama ya Juu, litafuatilia na kusajili kesi hiyo inayopinga matokeo ya uchaguzi wa rais kulingana na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu vinavyoongoza kesi kufanyika kwa haki.

Timu hiyo pia itachambua jukumu na uhuru wa mahakama katika kutathmini mzozo wa uchaguzi na kurejea hali ya siasa ya jamii kuelekea kufunguliwa hiyo kesi ya kupinga matokeo.

“Kufikia mwisho wa uangalizi wa kesi hiyo, waangalizi hao wataandika ripoti ya kina kwa kusudio la kuchangia zaidi katika taaluma, uhuru, uadilifu na kuwajibika kwa mahakama,” taarifa ya kikundi hicho imeeleza.

Mahakama hiyo kwa mara ya kwanza imetoa fursa kwa umma kupata nakala za nyaraka zilizowasilishwa katika kesi inayopinga matokeo ya uchaguzi ikiwa ni hatua ya kuimarisha uwazi.

Timu ya AJJF itakutana na Dr Ruto, Bw Odinga, na makamishna wa IEBC, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma na Mwanasheria Mkuu.

Takriban hoja nane zimewasilishwa kutaka kubatilishwa kwa ushindi wa Dr Ruto, na malalamiko kadhaa yakidai kuwepo ukiukaji mkubwa wa mchakato wa uchaguzi. Malalamiko mengine yanataka mahakama hiyo iangalie kuona iwapo Dr Ruto alifikia asilimia 50 na nyongeza ya moja inayohitajika kuweza kutangazwa mshindi.

Hoja nyingine inaitaka mahakama itupilie mbali malalamiko yanayopinga ushindi wa Dr Ruto. Mahakama itasikiliza kesi hiyo ya malalamiko kupinga matokeo ya uchaguzi na kutoa uamuzi Septemba 5.

Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African"

XS
SM
MD
LG