Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 12:54

Waasi 6 wa Mai-Mai wauawa DRC


Jeshi la DRC

Askari mmoja na waasi wa Mai-Mai sita wameuwawa katika mapambano Alhamisi upande wa mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) karibu na mpaka wa Uganda, jeshi la Congo limesema.

Kuanzia mwanzo wa mwaka 2017, wapiganaji wa Mai-Mai mara nyingi wamekuwa wakishambulia maeneo mbalimbali ya jeshi la Congo katika eneo.

Shirika la habari la AFP limeripoti kuwa mapambano ya hivi karibuni kati ya majeshi ya serikali na waasi yalianza katika majira ya saa mbili asubuhi, wakazi wa eneo la Kasindi, katika jimbo la Kivu Kaskazini, wamesema.

Kasindi ni sehemu ambapo kipo kituo kikuu cha forodha upande wa mashariki wa DRC na ambapo bidhaa nyingi zinazoingia nchini kutoka Uganda hupewa kibali.

“Tunasikitika kwa kifo cha askari, na wengine watatu waliojeruhiwa, na waasi sita wameuawa na wengine watatu wamekamatwa,” alisema msemaji wa jeshi katika eneo hilo ameeleza, Luteni Jules Tshikudi.

“Utulivu umerejea hivi sasa baada ya masaa kadhaa ya mapambano ambapo silaha nzito na nyepesi zilitumika, na Jeshi limeweza kulidhibiti eneo hilo,” aliongeza.

XS
SM
MD
LG