Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 18:10

Mahakama Zimbabwe yaanza kusikiliza rufani ya MDC


Maafisa wa polisi wakiimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya Kikatiba Harare, Jumatano, Agosti 22, 2018.

Mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe, imeanza kusikiliza rufaa iliyo wasilishwa na chama kikuu cha upinzani cha Movement for Democratic Change - MDC, kikitaka kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Julai, yaliyompa ushindi Rais-mteule Emmerson Mnangagwa.

Chama cha MDC, kinadai kwamba tume ya uchaguzi ilifanya udanganyifu katika kuhesabu kura kitendo kilicho mnufaisha Rais Mnangagwa wa chama kinachotawala ( ZANU-PF).

Mnangagwa alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika Julai 30 baada ya kupata asilimia 51 ya kura zilizopigwa na kumshinda mpinzani wake Nelson Chamisa wa MDC, aliyepata asilimia 44.3.

Chamisa na chama chake cha MDC, kilipinga matokeo ya uchaguzi huo.

Chamisa amesisitiza kuwa chama cha MDC kina ushahidi wa kutosha kwamba tume ya uchaguzi kwa ushirikiano na chama kinacho tawala cha ZANU-PF, kilifanya udanganyifu katika kuhesabu kura na kwamba ana imani mahakama ya kikatiba itafutilia mbali matokeo hayo na kuamrisha uchaguzi kufanyika upya.

Uchaguzi wa Julai 30, ulikuwa wa kwanza kutomshirikisha kiongozi wa muda mrefu wa nchi ya Zimbabwe, Robert Mugabe, aliyeondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi.


Facebook Forum

XS
SM
MD
LG