Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 15:06

Mugabe : Siwezi kuipigia kura ZANU-PF


Rais wa zamani Robert Mugabe
Rais wa zamani Robert Mugabe

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ameonyesha hasira Jumapili dhidi ya chama chake cha siasa alichokiasisi, na kusema hawezi kukipigia kura chama tawala cha ZANU-PF katika uchaguzi wa Jumatatu.

Huu ni uchaguzi wa kwanza katika kipindi cha miaka 38 ambapo Mugabe hatashiriki kama mkuu wa chama cha ZANU-PF. Alijiuzulu Novemba kufuatia shinikizo kutoka jeshini.

Naibu wake wa muda mrefu, Emmerson Mnangagwa (75) alichukua madaraka na hivi sasa anagombea nafasi ya urais.

"Sitawaunga mkono wale walio ninyanyasa,” amesema Mugabe, ambaye aliwakaribisha waandishi wa habari nyumbani kwake ikatika kitongoji wanakoishi matajiri.

Alipoulizwa ni mgombea gani atamchagua siku ya Jumatatu, Mugabe alionyesha kuwa na mashaka. Ijapokuwa kuna wagombea 23 waliojitokeza kugombea nafasi ya urais, hivi sasa wamebakia wagombea wawili, ikiwa Mnangagwa anakabiliwa na ushindani mkubwa wa kiongozi mpya wa chama kikubwa kuliko vyote cha upinzani, ambaye ni Nelson Chamisa (40).

“Siwezi kuipigia kura ZANU-PF,” amesema Mugabe. “Siwezi kuwapa kura wale ambao wamenifikisha hapa nilipo katika hali hii.”

Pia alionyesha kutokubaliana na wagombea wengine; “Pia nimesema, Ma (Joice) Mujuru na Ma (Thokozani) Khupe hawana cha kuleta kikubwa. Na alobakia ni Chamisa.”

Mugabe kwa hali zote akionyesha kupinga chama chake na kiongozi wake mpya, amesema, “Yalikuwa ni mapinduzi ya kijeshi ambayo yalipelekea yeye kupoteza madaraka.

Alilalamika namna alivyotendewa kwa zaidi ya miezi saba, akisema wanafamilia walikuwa wakisumbuliwa na kutishiwa,na kusikitika kuwa pensheni yake inayotolewa na serikali ni dola $460,000 na nyumba mbili.

XS
SM
MD
LG