Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 04:22

Mahakama ya Katiba yatupilia mbali madai ya upinzani Zimbabwe


Chini ya ulinzi mkali maafisa wa chama cha upinzani wakiwa wanapekuliwa wakati walipowasili mahakamani mjini Harare, Zimbabwe kusikiliza kesi ya uchaguzi waliofunguwa kupinga matokeo ya uchaguzi, Jumatano, Agosti 22, 2018,.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Ijumaa ameridhia uamuzi wa Mahakama ya Katiba uliothibitisha ushindi wake kufuatia uchaguzi mkuu, baada ya majaji kutupilia mbali madai ya upinzani yakitaka matokeo ya uchaguzi yafutwe kwa madai ya kuwa kulikuwa na wizi wa kura.

“Mara nyingine tena nasisitiza wito wangu wa kuimarisha amani na umoja kuliko suala lolote jingine,” Mnangagwa amesema katika ujumbe wake wa Twitter.

“Sote hivi sasa tuweke pembeni tofauti zetu. Ni wakati wa kusonga mbele kwa kushirikiana kwa pamoja.”

Mahakama ya juu Ijumaa imetupilia mbali ombi la upinzani wakitaka matokeo ya uchaguzi yabatilishwe kwa tuhuma za kuwa uchaguzi ulichakachuliwa na kumpa ushindi mrithi wa Robert Mugabe, Emmerson Mnangagwa.

“Katika uchambuzi wake wa mwisho, mahakama hiyo imegundua kuwa upinzani wameshindwa kuweka mbele ya mahakama hiyo ushahidi uliowazi, wa moja kwa moja, ambao unajitosheleza na uliyo na ukweli ”juu ya mapungufu ya uchaguzi huo, amesema Jaji Mkuu Luke Malaba katika uamuzi wake aliyo utoa katika Mahakama ya Katiba mjini Harare.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa walikuwa wametabiri kwa upana kuwa mahakama itafanya uamuzi dhidi ya kesi iliyo funguliwa na chama cha upinzani cha Democratic Change Party kupinga matokeo.

XS
SM
MD
LG