Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 22:12

Mahakama Ubelgiji yaamrisha jino la Lumumba kurudishwa Congo


Patrice Lumumba

Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo Patrice Lumumba jino lake linalohifadhiwa Ubelgiji, mahakama nchini humo imesema linapaswa kurudishwa kwao.

Binti yaka Lumumba ameiambia idhaa ya Ujerumani DW uamuzi wa mahakama kuwapa kitu pekee kilichokuwa kimebakia cha baba yao ulikuwa "ushindi mkubwa."

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vimeripoti kuwa Serikali ya Kongo imeupongeza uamuzi wa Mahakama ya Ubeljiji uliotolewa siku ya Alkhamisi.

Vinasema Waziri wa Haki za Binadamu wa Kongo, André Lite, amesema kurejeshwa kwa mabaki hayo, kutaiwezesha Kongo kumfanyia Lumumba mazishi ya kitaifa.

"Katika siku za hivi karibuni, serikali itachukuwa msimamo wa dhati. Naweza kusema kwamba kutafanyika mazishi rasmi ya kitaifa, sababu Patrice Emery Lumumba anastahili heshima hizo. Anatakiwa kuenziwa na taifa lake'', vyombo vya habari vimemnukuu waziri huyo.

Lumumba, aliyekuwa waziri mkuu wa Kongo baada ya uhuru kutoka kwa Ubeljiji 1960, aliuawa Januari 17 mwaka 1961 katika hali ya kutatanisha.

Jino lake lilichukuliwa na afisa mimosa wa polisi wa Ubelgiji aliyekuwa akisaidia kuuzika mwili wake.

Baada ya miaka mingi, afisa huyo alielezea kwamba mwili wa Lumumba uliunguzwa kwa kutumia tindikali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG