Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 02:17

Mahakama Nigeria yaongeza muda wa matumizi ya noti ya zamani


Noti za naira za Nigeria. Picha na Shirika la habari la REUTERS/Afolabi Sotunde/Maelezo /Maktaba.

Mahakama ya juu nchini Nigeria siku ya Ijumaa iliiamuru benki kuu kuongeza muda wa matumizi ya noti za zamani hadi Desemba 31, ambazo kuondolewa kwake kwenye mzunguko lilikuwa suala kuu katika uchaguzi baada ya kusababisha uhaba wa fedha taslimu, na kuenea ugumu wa maisha na hasira.

Muda uliokuwa umewekwa uliwakasirisha wanigeria wengi ambao walikuwa na njaa na uchovu, muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa taifa wa kumpata mtu atakayechukua nafasi ya rais Muhammadu Buhari. Uchaguzi huo ulishuhudia idadi ndogo ya asilimia 29 ya waliojitokeza kupiga kura.

Gavana wa zamani wa jimbo la Lagos Bola Tinubu wa chama tawala cha Buhari cha All Progressives Congress (APC) alichaguliwa katika nafasi urais kwenye upigaji kura ulifoanyika mwishoni mwa wiki.

Majimbo kumi na sita nchini Nigeria yalifungua kesi mahakamani, wakidai kwamba Wanigeria wengi wamekwama kubadilisha noti za zamani na wanahitaji muda zaidi ya tarehe 10 mwezi Februari wakati ambapo noti zote zitaacha kutumika kama sarafu halali katika mchakato mbaya wa ubadilishaji wa noti za zamani na mpya zaidi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG