Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 08:24

Nigeria: Vyombo vya habari vilivyopeperusha ripoti ya BBC kuhusu ujambazi vyalazimishwa kulipa faini


Waziri wa habari wa Nigeria, Lai Mohammed. Picha ya AP
Waziri wa habari wa Nigeria, Lai Mohammed. Picha ya AP

Tume inayofuatilia utangazaji nchini Nigeria imetoa adhabu ya faini ya naira milioni 5, sawa na dola 12,013 kwa kituo cha televisheni Multichoice Nigeria Ltd, na kwa vyombo vingine vya habari kwa kupeperusha ripoti ya BBC.

Tume hiyo ilisema ripoti hiyo “inatukuza harakati za majambazi na inadhoofisha usalama wa taifa."

Tume hiyo ya kitaifa inayofuatilia matangazo ilisema Jumatano katika taarifa kwamba vyombo hivyo vya habari vinatakiwa kulipa faini hiyo ifikapo tarehe 30 Agosti.

Imetoa pia adhabu ya faini kwa kituo cha televisheni cha Trust TV, sehemu ya mtandao unaomiliki gazeti la Nigeria lenye umaarufu Daily Trust, kwa ripoti yake kuhusu ujambazi.

“Tume inataka kutumia fursa hii kwa kushauri watangazaji kuwa makini na waangalifu katika kuchagua na kupitisha maudhui ambayo yanahatarisha usalama wa taifa la Nigeria,” tume hiyo(NBC) imesema katika taarifa.

Daily Trust imenukuu uongozi wake ukisema, “Tunataka kusema kwamba kama kituo cha televisheni, tunaamini tulifanya kazi yetu kwa maslahi ya umma kwa kutoa mwanga juu ya suala hilo gumu la ujambazi.”

BBC nayo imesema katika taarifa yake kupitia barua pepe“ habari hii ina manufaa makubwa kwa umma na BBC inaunga mkono uandishi wake.”

Multichoice Nigeria Ltd haikutoa mara moja maelezo juu ya adhabu hiyo.

XS
SM
MD
LG