Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 19:42

Mawakili wa CUF- Maalim wadai mahakama haizuiwi na bunge


Katibu Mkuu wa Chama cha upinzani CUF Seif Sharif Hamad
Katibu Mkuu wa Chama cha upinzani CUF Seif Sharif Hamad

Wabunge wa viti maalum wa chama cha upinzani CUF nchini Tanzania, wamefikisha malalamiko yao mahakamani na hata hivvyo wako njiapanda.

Wako njiapanda kutokana na pingamizi la maombi yao ya kusimamisha uapishwaji wa wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao.

Wakili Kibatala alifafanua kuwa kifungu walichokitumia kufungua maombi hayo ni sahihi huku akirejea kesi mbalimbali zilizokwisha kuamuliwa na Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani akidai zilihalalisha matumizi ya kifungu hicho.

Kuhusu hoja ya kuzuia Bunge kutekeleza majukumu yake, alidai kuwa mahakama ndicho chombo cha kutoa haki na kwamba hakuna kanuni ya kisheria inayoizuia kutoa haki na kwamba hakuna kanuni ya kisheria inayoizuia kutoa haki kwa mambo yanayohusiana na Bunge na kwamba imekuwa ikifanya hivyo.

Kuhusu kuwajumuisha wajibu maombi wengine kwenye kesi ya msingi alidai kuwa upo uamuzi wa kuteuliwa kwa wabunge wapya uliofanyika wakiwa tayari wameshafungua kesi ya msingi na kwamba maelezo ya jambo hilo yako kwenye hati ya kiapo.

Waombaji hao ni Miza Bakari Haji na wenzake saba wakati wajibu maombi ni Katibu wa Bunge, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bodi ya Wadhamini wa CUF na wabunge wateule wanane.

Mbali na Miza, waombaji wengine katika maombi hayo ni Saverina Silvanus Mwijage, Salma Mohamed Mwassa, Raisa Abdallah Musa, Riziki Shahari Mngwali, Hadija Salum Al-Qassmay, Halima Ali Mohamed na Saumu Heri Sakala na madiwani Elizabeth Alatanga Magwaja na Layla Hussein Madib.

Kutokana na pingamizi hilo, mahakama ililazimika kusitisha usikilizwaji wa maombi ya msingi hivyo kusikiliza kwanza hoja za mapingamizi ya awali yaliyowasilishwa na wajibu maombi hayo ili kuyatolea uamuzi kabla ya kuendelea na maombi hayo.

Usikilizwaji wa maombi hayo sasa unategemea uamuzi wa mapingamizi hayo utakaotolewa Ijumaa na Jaji Lugano Mwandambo.

Wabunge hao walifungua maombi Mahakama Kuu wakiomba itoe amri ya zuio kwa Bunge ili wabunge wapya wasiapishwe, wakati wakisubuiri kesi waliyoifungua kupinga kufukuzwa uanachama wa chama hicho kusikilizwa.

Lakini inakabiliwa na pingamizi la awali kutoka kwa wajibu maombi, wakiiomba mahakama hiyo iyatupilie mbali kwa madai kuwa ni batili na kuwasilisha hoja nne kuyakosoa, jambo ambalo limefanya yabaki njia panda.

Lakini Tume ya Uchaguzi (NEC) na Bunge waliowakilishwa na jopo la mawakili wanane wa serikali wakiongozwa na Wakili wa serikali mkuu, Gabriel Malata katika pingamizi lao wamewasilisha hoja tatu, moja wakidai kuwa maombi hayo ni batili kwa kuwa yamefunguliwa kwa kifungu kisicho sahihi.

Walidai kuwa kifungu cha 2(3) Sheria ya Mamlaka ya Mahakama Kuu kutumia sheria za nje hususan za Uingereza (Jala) siyo sahihi kwani hicho kinatoa ridhaa kwa mahakama kutumia sheria za nje pale ambako kunakuwa hakuna kifungu rasmi katika sheria za nchi.

Malata alisema walipaswa kuonyeshwa kifungu rasmi katika sheria za Uingereza kinachotumika kulingana na mazingira ya maombi yao.

Katika hoja nyingine, Malata alidai kuwa nafuu wanazoziomba haziwezi kutolewa na mahakama hiyo kwa kuwa zinalenga kwenda kuzuia utekelezaji wa majukumu ya kikatiba ya mhimili mwingine (Bunge).

Katika hoja ya tatu ya pingamizi hilo alidai kuwa maombi hayo ni ya usumbufu na matumizi mabaya ya mwenendo wa mahakama kwa kuwa watoa maombi wanaomba nafuu kwa jambo moja katika mamlaka mbili tofauti.

XS
SM
MD
LG