Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:47

Madaktari wapendekeza Malkia Elizabeth awekwe katika uangalizi wa kiafya


Malkia wa Uingereza Elizabeth
Malkia wa Uingereza Elizabeth

Kasri ya Buckingham imetoa taarifa ikieleza wasiwasi juu ya afya ya Malkia Elizabeth mwenye umri wa miaka 96 baada ya kufanyiwa tathmini ya afya yake Alhamisi.

Taarifa hiyo ilisema madaktari wa mfalme wa Uingereza wamependekeza awekwe katika uangalizi wa kiafya. Imesema Malikia “yuko vizuri” katika nyumba yake ya Balmoral huko Scotland, makazi yake wakati wa majira ya joto.

Malkia alifuta mkutano wa Jumatano aliokuwa anakutana na Baraza la Privy, kikundi cha karibu yake, washauri wake wanaoaminika sana. BBC imeripoti Alhamisi kuwa Prince Charles na wanafamilia wengine wa ufalme huo wanasafiri kuelekea Balmoral ili wawe pamoja na Malkia.

Kutoka katika akaunti yake ya Twitter, Waziri Mkuu Liz Truss alisema “nchi nzima” ina “wasiwasi mkubwa” kwa habari hizo. Aliongeza kuwa, “Fikra zangu – na fikra za watu wote kote Uingereza – ziko pamoja na mtukufu Malkia na familia yake wakati huu.”

Malkia alimteua Truss kuwa waziri mkuu huko Balmoral Jumanne, badala ya kusafiri kwenda London kwa tukio hilo. Katika kipindi cha miaka 70 ya utawala wake Malkia amekuwa na kawaida ya kukutana na waziri mkuu mpya katika Kasri ya Buckingham.

Baadhi ya taarifa katika repoti hii inatokana na shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG