Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 18:10

Macron aahidi msaada wa dola milioni 36 kwa DRC, atishia vikwazo kwa watakaovuruga amani


Marais Emmanuel Macron wa Ufaransa (Kushoto) na mwenzake Felix Tshisekedi wa DRC (Kulia) wahutubia waandishi wa habari mjini Kinshasa.
Marais Emmanuel Macron wa Ufaransa (Kushoto) na mwenzake Felix Tshisekedi wa DRC (Kulia) wahutubia waandishi wa habari mjini Kinshasa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumamosi ameahidi msaada wa Euro milioni 34 (Dola milioni 36) kwa eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lililokumbwa na mzozo na kusema kuwa upande wowote unaotaka kuvuruga juhudi za amani huko unapaswa kukabiliwa na vikwazo.

Macron alikuwa akizungumza wakati wa ziara rasmi nchini humo, ambako mitazamo ya uungaji mkono wa Ufaransa kwa nchi jirani ya Rwanda imechochea hisia za chuki dhidi ya Ufaransa wakati maeneo ya mashariki yanapambana na mashambulizi ya kundi la waasi la M23 ambalo Kongo inaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono. Rwanda inakanusha hili.

Ufaransa hapo awali ilijiunga na Umoja wa Mataifa, Kongo na nchi nyingine katika kuishutumu Rwanda kwa kuunga mkono M23, lakini Macron aliulizwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa kulaani vikali zaidi Rwanda.

"Nimezungumzia wazi sana kuhusu kulaani kundi la M23 na wale wanaoiunga mkono," Macron alisema.

Mchakato wa amani uliosimamiwa na mataifa yenye nguvu katika kanda hiyo, mwezi Novemba hadi sasa umeshindwa kukomesha mapigano, lakini Macron alisema ana imani na mpango huo.

"Kama hawataiheshimu, basi ndiyo, kunaweza kuwa na vikwazo," alisema bila kutaja chama upande wowote.

Kongo ilishuhudia maandamano madogo madogo kabla ya ziara ya Macron - dalili za hisia za chuki dhidi ya Wafaransa katika sehemu za Afrika zinazozungumza Kifaransa, ambazo anajaribu kuzikabili katika ziara hii ambapo ameelezea maono ya aina mpya ya ushirikiano na bara hilo.

XS
SM
MD
LG