Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:40

Macron azungumza na Kagame na Tshisekedi, asifu "makubaliano ya kusitisha mapigano DRC kuanzia Jumanne"


PICHA YA MAKTABA: Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.
PICHA YA MAKTABA: Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, akiwa nchini DRC, kituo cha mwisho cha ziara yake barani Afrika, amesema kuwa pande zote zinazozozana katika mgogoro wa kiusalama unaokumba mashariki mwa nchi hiyo, zitaheshimu makubaliano ya usitishaji wa mapigano.

Wakati wa mazungumzo na Rais wa Angola Joao Lourenco na Rais wa DRC Felix Tshisekedi, pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Macron alisema wote "wameahidi uungaji mkono wa wazi " kwa usitishaji mapigano Jumanne ijayo, kama inavyotarajiwa katika kalenda ya matukio iliyopatanishwa na Angola.

Ziara ya Macron barani Afrika ina lengo la kurejesha uhusiano uliodorora.

Wakati huo huo, Brussels ilisema Jumamosi kuwa inazindua "operesheni ya angani" ili kupeleka misaada mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyokumbwa na mzozo.

Operesheni hiyo, iliyopewa jina la “Daraja la angani” italenga zaidi Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako mapigano na kundi la waasi la M23 yamewakosesha makazi zaidi ya watu 600,000.

Operesheni hiyo "itawasilisha msaada wa kibinadamu kwa njia ya vifaa vya matibabu na lishe pamoja na vitu vingine vya dharura", taarifa ya Tume ya Ulaya ilisema.

EU ilisema pia itatoa Euro milioni 47 kupitia washirika wa kibinadamu kwa mahitaji ya haraka kama vile lishe, huduma za afya, makazi na maji.

"EU iko tayari kutumia njia zote zinazohitajika kusaidia wafanyakazi wa kibinadamu, ikiwa ni pamoja na vifaa na ndege, ili kukidhi mahitaji ya watu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo," alisema kamishna wa EU wa usimamizi wa mgogoro Janez Lenarcic.

XS
SM
MD
LG