Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:12

Maandamano kupinga mapinduzi ya kijeshi Myanmar yaingia siku ya tano


Waandamanaji wakiwa mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Yangon Februari 10, 2021, wakipinga mapinduzi ya kijeshi yaliyo fanyika Februari 1, nchini Myanmar (Photo by Sai Aung Main / AFP)
Waandamanaji wakiwa mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Yangon Februari 10, 2021, wakipinga mapinduzi ya kijeshi yaliyo fanyika Februari 1, nchini Myanmar (Photo by Sai Aung Main / AFP)

Maandamano ya nchi nzima kupinga mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopiya kuiondoa serikali ya kiraia yameingia siku ya tano Jumatano pamoja na jeshi hilo kuongeza matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji.

Ripoti zinaeleza kuwa vikosi vya usalama vilifyatua risasi za mpira na maji ya kuwasha kwa waandamanaji katika juhudi za kutawanya kundi la watu na kusababisha baadhi ya watu kuumia.

Daktari mmoja ambaye aliyewatibu waandamanaji katika hospitali ya Naypyitaw ameiambia VOA kwamba takriban waandamanaji wawili walipata majeraha yanayo aminika kuwa yametokana na risasi za moto, mmoja akiwa na jeraha kichwani na mwingine kifuani.

Ikiwa ni zaidi ya wiki moja baada ya jeshi kumshikilia kiongozi wa taifa hilo Aung San Suu Kyi na maafisa wengine wa juu wa serikali ya kiraia jeshi limeongeza harakati zake kwa kuvamia makao makuu ya chama cha kiongozi huyo cha National League for Democracy – NLD – yaliyoko Yangon Jumanne usiku.

XS
SM
MD
LG