Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 12:13

Waalimu wajiunga na kampeni dhidi ya mapinduzi ya kijeshi Myanmar


Wafanyakazi wa afya wakipinga mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar.

Waalimu nchini Myanmar Ijumaa wamekuwa kundi la hivi karibuni kujiunga na kampeni ya kiraia ya utovu wa nidhamu.

Wakati huohuo baadhi ya wahadhiri wamekataa kufanya kazi au kushirikiana na viongozi wakipinga kitendo cha jeshi kuchukua madaraka kwa nguvu.

Kampeni ya kiraia ya kutotii sheria ilianza na wafanyakazi wa afya muda mchache baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Jumatatu.

Na kuanzia wakati huo kampeni hiyo ilishika kasi na kujumuisha wanafunzi, makundi ya vijana na baadhi ya wafanyakazi katika sekta za serikali na binafsi.

Wakiwa wamevaa vitambaa vyekundu huku wakibeba mabango katika maandamano, waalimu wengi walikusanyika mbele ya majengo ya chuo kikuu cha elimu cha Yangon.

Maandamano Japan yakilaani mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Aung San Suu Kyi, Mynmar.
Maandamano Japan yakilaani mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali ya Aung San Suu Kyi, Mynmar.

“Hatutaki mapinduzi haya ya kijeshi ambayo yalinyakua madaraka kinyume cha sheria kutoka kwa serikali yetu iliyochaguliwa”, mhadhiri New Thazin Hlaing amesema.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG