Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 20:44

Aung San Suu Kyi na wenzake wamewekwa kizuizini Myanmar


Aung San Suu Kyi, kiongozi wa Myanmar

Hatua hiyo imekuja baada ya siku kadhaa za kuongezeka mvutano kati ya serikali ya kiraia na jeshi lenye nguvu ambalo lilichochea hofu ya mapinduzi baada ya uchaguzi ambao jeshi linasema ulijaa ulaghai

Kiongozi wa Myanmar, Aung San Suu Kyi na wenzake kutoka chama tawala wamewekwa kizuizini na Jeshi kufuatia ukamataji uliofanywa asubuhi ya Jumatatu kwa saa za huko msemaji wa chama cha kitaifa cha Democracy amesema Jumatatu.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku kadhaa za kuongezeka mvutano kati ya serikali ya kiraia na jeshi lenye nguvu ambalo lilichochea hofu ya mapinduzi baada ya uchaguzi ambao jeshi linasema ulijaa ulaghai.

Msemaji Myo Nyut ameliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu kwamba Suu Kyi, Rais Win Myint na viongozi wengine walichukuliwa mapema asubuhi kwa saa za huko. Ameongeza kuwa ninataka kuwaambia watu wetu wasijibu kwa haraka na ninawataka wachukue hatua kulingana na sheria.

Njia za simu kwenda Naypyitaw, mji mkuu hazikuweza kupatikana katika majira ya asubuhi kwa saa za huko siku ya Jumatatu. Msemaji wa jeshi hakujibu simu zinazomtaka kutoa maoni yake kuhusiana na suala hili.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG