Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 03:46

Rais Lukashenko aapishwa kushikilia madaraka kwa muhula wa sita


Belarusian President Alexander Lukashenko speaks during a meeting with the country's political activists in Minsk, Belarus, Sept. 16, 2020.

Hata baada ya maandamano ya wiki kadhaa yakimtaka ajiuzulu, Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, Jumatano, ameapishwa kuongoza kwa muhula wa 6 baada ya kuwa madarakani kwa miaka 26.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hafla hiyo imefanyika kimya kimya kinyume na siku za nyuma labda kutokana na malalamiko mengi yaliowasilishwa na upinzani, pamoja na baadhi ya mataifa ya kigeni, kuwa uchaguzi uliofanyika Agosti 9 ulikuwa na udanganyifu.

Upinzani hata hivyo umepuuzia kuapishwa kwa Lukashenko na badala yake kutaka maandamano dhidi ya utawala wake yaendelee na ambayo yamekuwa yakifanyika kwa wiki 6 sasa.

Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya wanaendelea kutathmini kuhusu vikwazo dhidi ya maafisa waliohusika kwenye uchaguzi huo pamoja na maafisa wa usalama ambao wamekuwa wakifanya misako dhidi ya waandamaji.

Baada ya kuapishwa, Lukashenko mwenye umri wa miaka 66 amesema kuwa taifa lake linahitaji usalama na maelewano wakati likikabiliana na janga la kimataifa, akionekana kuashiria janga la virusi vya corona.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG