Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:13

Bendera zatumika kuweka kumbukumbu ya waliokufa na COVID-19 Marekani


Bendera zilizowekwa na wanaharakati
Bendera zilizowekwa na wanaharakati

Wanaharakati Jumanne waliweka vibendera 20,000 vya Marekani kwenye eneo la Washington Monument hapa mjini Washington DC, wakati Marekani ikifikisha vifo 200,000 kutokana na COVID-19.

Vibendera hivyo ni kumbukumbu ya watu hao waliokufa kutokana na virusi vya corona tangu mlipuko huo utokee nchini mwanzoni mwa mwaka 2020.

Kwa mujibu wa wanaharakati walioweka vibendera hivyo kila kibendera kiliwakilisha watu 10 waliokufa kutokana na COVID-19.

Kwenye hafla hiyo iliyojumuisha watu kutoka dini mbalimabli, Spika wa Baraza la Wawakilishi Marekani Nancy Pelosi alizungumza na kusema kuwa idadi hiyo kubwa ya vifo ingezuilika.

Pia alitoa wito kwa taifa kuzingatia sayansi ili kuepuka hasara kama hiyo katika siku zijazo.

Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani anaeshugulikia magonjwa ya kuambukizana Dkt Anthony Fauci mwezi Aprili alisema kuwa idadi ya vifo ilikuwa takriban 60,000.

Kwa upande wake Rais Donald Trump akifananisha virusi hivyo na vile vya homa ya kawaida mwezi Mei, alisema kuwa idadi ya vifo huenda ilikuwa kati ya 75,000 na 100,000.

Wataalam wa afya kutoka chuo kikuu cha Washington wanasema sasa kuwa huenda idadi ya vifo hapa Marekani ikafikia 410,000 kufikia mwishoni mwa mwaka. Kufikia sasa Marekani inaongoza kwa idadi ya vifo kutokana na virusi hivyo ulimwenguni.

XS
SM
MD
LG