Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 00:26

Rais wa TLS Lissu kuendelea kupigania demokrasia Tanzania


Tundu Lissu akiwa na wabunge wenziwe katika mashauriano ya kitaifa ndani ya bunge
Tundu Lissu akiwa na wabunge wenziwe katika mashauriano ya kitaifa ndani ya bunge

Kaka yake mkubwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Alute Mughwai, amesema ameteta na mdogo wake kwa njia ya simu na kumweleza atarejea kwenye mapambano ya kuilinda demokrasia Tanzania.

Hili limetokea siku moja baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kurejea nchini na kueleza mwenendo wa afya ya Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi akiwa yuko katika shughuli za bunge Jijini Dodoma. Mpaka hivi sasa Lissu anapatiwa matibabu nchini Kenya.

Lissu kuendelea kupigania demokrasia Tanzania

“Ujasiri, hamasa na kujiamini hakujaondoka. Ameniambia piganieni haki zenu na haki za Watanzania, piganieni uhuru wa kujieleza, uhuru wa kutoa maoni na hakikisheni kunakuwa na demokrasia na utawala wa sheria katika Tanzania,” alisema Mughwai akimnukuu Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Lissu uliofanyika jijini Arusha.

“Kwanza niwaambie tu Rais wetu wa TLS anaendelea vizuri sana, anawatakia mfanye mkutano huu kwa mafanikio. Kabla sijaingia katika ukumbi huu, nilijaribu kumpigia (simu) mke wake ambaye ni shemeji yangu, lakini badala ya kuipokea, alimpatia Lissu nikazungumza naye,” alisema Mughwai ambaye pia ni wakili.

Amesema alipokuwa akizungumza naye kwa simu, Lissu alimhakikishia kuwa afya yake imeimarika, isipokuwa maumivu katika majeraha ya risasi katika eneo la nyonga na miguuni.

“Rais wetu ufahamu wake umerudi katika hali ya kawaida, anajieleza vizuri, maana yake ni kuwa eneo lote la kiunoni kwenda kichwani yuko sawa, isipokuwa kuanzia kiunoni kwenda miguuni ndilo eneo lililoumizwa sana," alisema Mughwai.

TLS walaani mashambulizi ya Lissu

“Sote tunawalaani majahili hawa wasiojulikana, ambao walikusudia kupoteza uhai wake. Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani basi aliye juu yetu? Bila shaka hakuna, tunaamini siku chache zijazo ataungana nasi kuendelea kuipigania nchi yetu,” aliongeza Mughwai.

Kwa mujibu wa Mughwai ambaye ndiye msemaji wa familia hadi sasa familia yake Lissu haijaelewa kwa uwazi masharti na nia iliyo nyuma ya tamko la Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Mughwai, alishangazwa na wito wa Serikali kupitia kwa Waziri Ummy juu ya matibabu ya mbunge huyo, ambaye anastahili haki zote za kutibiwa na Serikali, hasa ikizingatiwa alishambuliwa na kuumizwa akiwa katika eneo lake la kazi.

“Tunashirikiana tangu mwanzo wa tukio hili na Chadema, TLS na wasamaria ambao wengi ni wananchi na watu wengine wa kawaida, wacha tusiwakatishe tamaa hawa waliojitokeza mwanzo kuwa nasi, hawa wenye masharti wasubiri,” alisema Mughwai.

Ummy afafanua

Waziri Ummy alilazimika kufafanua kauli yake kupitia mtandao wa Twitter, Jumamosi akisisitiza kuwa Serikali haiwezi kugharamia matibabu ya Lissu pasipo kupata ridhaa ya familia kwa kuwa kiongozi huyo alitolewa katika utaratibu wa matibabu baada ya kupelekwa Nairobi.

Kauli yake hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kukaririwa na vyombo vya habari akihoji utaratibu unaotakiwa na Serikali ili iweze kumtibia Lissu, jambo ambalo alidai kuwa halikuwahi kufanyika kwa wabunge wengine.

XS
SM
MD
LG