Vyama vikuu vya upinzani huko Tanzania vinadai kwamba wananchi wamechoshwa na maisha magumu pamoja na sera za chama tawala cha CCM.
Mgombea kiti cha rais kwa niaba ya chama cha CUF Profesa Ibrahim Lupumba akizungumza na Sauti ya Amerika amesema kutokana na mahitaji makubwa ya wananchi kwa wakati huu ni muhimu sana kukuza uchumi na kuongeza ajira.
Ili kufikia malengo hayo anasema "inahitaji kuwekeza katika miundo mbinu hususan kua na umeme wa hakika,na umeme uweze kusambazwa katika vijiji vikubwa vikubwa kusudi watu waweze kupata fursa kuanzisha viwanda vidogodogo vinavyoweza kutoa ajira", amesema kiongozi wa chama cha wananchi CUF, Profesa Lipumba.