Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:03

Uchaguzi Tanzania 2010


Uchaguzi Tanzania 2010
Uchaguzi Tanzania 2010

Wananchi wa Tanzania watapiga kura Oktoba 31, 2010 katika uchaguzi mkuu kuchagua rais, wabunge na madiwani katika serikali za mikoa. Uchaguzi huu ni wa nne wa vyama vingi tangu Tanzania irejee katika siasa za vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Wananchi wa Tanzania watapiga kura Oktoba 31, 2010 katika uchaguzi mkuu kuchagua rais, wabunge na madiwani katika serikali za mikoa. Uchaguzi huu ni wa nne wa vyama vingi tangu Tanzania irejee katika siasa za vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa chama tawala cha CCM anajaribu kupata awamu ya pili na ya mwisho baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa mwaka 2005. Rais Kikwete anakabiliwa na upinzani kutoka vyama vingine sita ambavyo vina wagombea urais. Wagombea hao ni pamoja na Dr. Ibrahim Lipumba wa chama cha CUF, Dr. Wilbroad Slaa wa CHADEMA, Mutamwega Mugahywa wa chama cha TLP, Peter Kuga Mziray wa ATPT Maendeleo, Hashim Rungwe wa NCCR-Mageuzi na Fahmi Dovutwa wa chama cha UPDP.

Uchaguzi huo pia unaandamana na uchaguzi wa rais wa Zanzibar ambako Rais wa sasa Amani Abeid Karume kutoka chama cha CCM anamaliza awamu yake ya pili ya uongozi. Wanaowania kuchukua nafasi hiyo ni Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Ali Mohamed Shein wa CCM akipambana na Seif Shariff Hamad wa CUF ambaye anagombania urais wa visiwa hivyo kwa mara ya nne.

Katika uchaguzi huu pia wananchi watapiga kura kuchagua wabunge 236 katika bunge la Jamhuri ya Muungano lenye jumla ya wajumbe 324, na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lenye jumla ya wajumbe 81. Maelfu ya wagombea wengine wanawania nafasi za udiwani katika serikali za mikoa na wilaya.

Uchaguzi wa mwaka huu Tanzania unafanyika chini ya sheria mpya ya gharama ya uchaguzi ambayo inafuatilia mwenendo wa wagombea katika matumizi yao ya fedha kwa shabaha ya kuondoa utumiaji rushwa kuomba kura kutoka kwa wananchi.

XS
SM
MD
LG