Takriban watu 11,300 walikufa wakati mabwawa mawili ya maji yalipovunja kingo, kufuatia dhoruba iliyopewa jina la Daniel wiki iliyopita, na kusababisha maji mengi zaidi kusomba watu na mali katika jiji hilo, kulingana na shirika la misaada la Red Crescent.
Watu wengine 10,000 hawajulikani walipo, na wanadhaniwa kuwa wamekufa. Siku ya Jumapili, basi lililokuwa limebeba waokoaji 19 wa Ugiriki liligongana na gari lililokuwa limewabeba raia watano wa Libya kwenye barabara kati ya miji ya Benghazi na Derna.
Raia watatu wa Libya waliokuwa kwenye gari hilo pia waliuawa. Mkasa huo wa mafuriko umeleta umoja adimu kwa Libya yenye utajiri wa mafuta, ambayo imegawanyika kati ya serikali hasimu za mashariki na magharibi mwa nchi hiyo, zinazoungwa mkono na vikosi mbalimbali vya wanamgambo na jumuiya za kimataifa.
Wakaazi kutoka miji ya karibu ya Benghazi na Tobruk wamejitolea kuwapa hifadhi waathiriwa, huku watu wengi wakijitolea kuwatafuta manusura waliofukiwa chini ya vifusi.
Forum