Wakaazi wa Derna mashariki mwa Libya walikuwa wakitahmini hasara walizopata kutokana na mafuriko yaliyoharibu maeneo mengi ya mji huo wa pwani huku juhudi za kuwatafuta watu wasiojulikana walipo zikiendelea siku ya Jumamosi kwa siku ya sita huku miili zaidi zikitolewa baharini.
Mtaa wa Kati ambao hapo awali ulikuwa kitovu cha shughuli za kiuchumi huko Derna ukiwa na maduka, kwa kiasi kikubwa haukuwa na watu, huku sauti ya upepo unaovuma ndio ilikua inasikika pekee yake kupita kwenye majengo yaliyoharibika huku watu wachache wakiwa wamekaa barabarani wakiwana majonzi, wakinywa kahawa na kuchunguza uharibifu.
Mwalimu mwenye umri wa miaka 44 Tarek Faheem al-Hasadi, ambaye mke wake na wajukuu watano waliuawa katika mafuriko, Jambo la kwanza ninaloogopa ni kwamba hii itachukua muda mrefu,. Yeye na mwanawe walinusurika kwa kupanda juu ya paa.
Hili linahitaji uvumilivu na ninaogopa kwamba msaada unaokuja ni wa muda mfupi, alisema akitokwa na machozi, akiwa amesimama mbele ya nyumba yake iliyoharibiwa lakini akiongeza kuwa amedhamiria kutoondoka eneo hilo.
Forum