Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:22

Kumetokea mashambulizi ya Guruneti Bujumbura, Burundi


Guruneti tatu zimerushwa katikati mwa jiji la Bujumbura Jumatano mchana na kusababisha majeraha kwa watu wasiopunguwa wanane.

Polisi inasema kuwa watu wawili wamekamatwa wanaohusishwa na kutekeleza shambulizi hilo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Pamoja na tukio hilo, hali ya utulivu imekuwa ikishuhudiwa katikati mwa jiji la Bujumbura kwa miezi kadhaa,.

Visa vya aina hiyo vimekuwa vikiripotiwa katika sehemu nyingine za vitongoji vya mji huo tofauti na katikati mwa mwa jiji la Bujumbura.

XS
SM
MD
LG