Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 01:53

Maandamano ni haki ya kikatiba, Chadema yajitetea


Mmoja ya maandamano makubwa ya Chadema yaliyofanyika Juni 20, 2017.

Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) limeibuka likitaka uchunguzi wa haraka ufanyike, huku likitaja makundi matatu yanayopaswa kulaumiwa kwa kifo cha mwanafunzi huyo.

Mwenyekiti wa Tahliso, George Mnali alisema makundi hayo hayawezi kukwepa lawama kuhusu kifo cha binti huyo kilichotokea Februari 16 kwa kuwa pasipo wao kuandamana asingefikwa na umauti.

Madai haya yametolewa Jumamosi wiki mbili baada ya mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini kuuwawa kwa kupigwa risasi suala kuhusu kifo chake limeibuka upya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amejibu tuhuma hizo kwa kusema anashangazwa na lawama zinazotolewa na shirikisho hilo akidai huenda wametumwa.

Alisema kuwa alitegemea kwamba Tahliso kama wasomi, walipaswa kufahamu kuwa maandamano ni haki ya kikatiba.

“Hawa ni wasomi gani ambao hawafahamu kuwa maandamano yapo kikatiba na Sheria ya Vyama vya Siasa inaruhusu jambo hilo. Nadhani wangejikita kujua chanzo cha maandamano na ningeona wako sahihi kama wangemuelekezea lawama hizo mkurugenzi wa Kinondoni aliyechelewesha kutoa hati za viapo kwa mawakala,” alisema.

Mrema alihoji pia ni nini hasa kilichowachelewesha Tahliso kutoa tamko hilo hali ya kuwa tukio la mauaji ya Akwilina Akwilini limetokea wiki mbili zilizopita.

Akwilina aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT, aliuwawa kwa kupigwa risasi eneo la Kinondoni Mkwajuni wakati polisi wakitawanya maandamano ya wafuasi wa Chadema wakiwa na viongozi wao waliokuwa wakielekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kinondoni kudai hati za viapo vya mawakala wake.


Facebook Forum

XS
SM
MD
LG