Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 19:36

Korea Kaskazini yakaidi vikwazo vipya vya UN


Balozi wa Marekani Nikki Haley akiongea na Balozi wa China UN Liu Jieyi baada ya kura kupitisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini
Balozi wa Marekani Nikki Haley akiongea na Balozi wa China UN Liu Jieyi baada ya kura kupitisha vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imetoa ujumbe mpya ikipinga vikwazo vipya vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kutokana na muendelezo wa programu za nyuklia na makombora za siri.

Katika taarifa iliyotolewa mapema leo kupitia shirika la habari la nchi hiyo KCNA, Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imesema kwamba vikwazo vipya vinalengo la kuleta madhara kwa taifa hilo na watu wake.

Imeongeza kuwa vikwazo hivyo vinalengo la kuzuia kabisa ustawi wa nchi hiyo kiuchumi.

Han Tae Song, ambaye ni balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa, alipokuwa katika mkutano wa kudhibiti silaha za maangamivu uliofadhiliwa na UN mjini Geneva, amesema kwamba, Marekani itakabiliwa na “matatizo makubwa” kwa kuchukuwa jukumu la kuwa mstari wa mbele kushinikiza vikwazo vipya kupitia baraza la usalama.

Serikali ya Korea Kaskazini itaongeza juhudi mara mbili kuwa na nguvu zenye kuweza kuulinda uhuru wa nchi hiyo na haki yake yakuwepo kama taifa, wizara hiyo imesema.

Hatua ya vikwazo vipya dhidi ya Korea Kaskazini ni kujibu jaribio la nyuklia ambalo linauwezekano wa kuwa ni bomu la hydrojeni lililofanywa na nchi hiyo Septemba 3.

Tume ya Korea Kusini inayosimamia tahadhari na usalama wa nyuklia imesema Jumatano kuwa imebaini kuwa chembechembe za miale ya nyuklia baada ya jaribio hilo la Korea Kaskazini lakini imeshindwa kuthibitisha iwapo bomu hilo lilikuwa la hydrojeni, kama ilivyokuwa imedaiwa na Pyongyang.

XS
SM
MD
LG