Picha mbalimbali zikionyesha jinsi makundi mbalimbali yanayoshiriki katika mchuano ya Kombe la Dunia yalivyoweza kukonga nyoyo za washabiki wao katika mechi zinazoendelea nchini Russia.
Kombe la Dunia Russia 2018 : Matukio ya timu zilizopambana katika michuano ya awali
HABARI KATIKA PICHA: Timu mbalimbali katika makundi zilizoshiriki katika kombe la dunia

1
Madaktari wa timu ya Belgium wakimsaidia mchezaji Romelu Lukaku kupata huduma ya kwanza wakati wa mechi ya Kundi G kati ya Belgium and Tunisia katika uwanja wa Spartak Moscow, Russia, Jumamosi, Juni 23, 2018.

2
Mchezaji wa timu ya Uingereza Jesse Lingard akiwatoka wachezaji wa Panama Armando Cooper, kushoto, na Blas Perez wakati wa mechi za kundi G kati ya Uingereza na Panama katika uwanja wa Nizhny Novgorod, huko mji wa Nizhny Novgorod , Russia, Jumapili, Juni 24, 2018.

3
Mchezaji wa Argentina Lionel Messi akisheherekea ushindi baada ya mchezo wa kundi kati ya Argentina and Nigeria katika uwanja wa St. Petersburg katika mji wa St. Petersburg, Russia, Jumanne, Juni 26, 2018. Argentina ilishinda 2-1.

4
Mchezaji wa Argentina's Marcos Rojo, wapili kulia, akifunga goli la pili wakati wa mchuano kati ya Argentina and Nigeria.