Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 22, 2025 Local time: 03:00

Kiongozi wa Palestina asema amani haiwezi kupatikana bila suluhisho la mataifa mawili


Kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas
Kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas

Kiongozi wa Palestina Mahmud Abbas alisema Alhamisi kwamba hakuwezi kuwa na amani katika Mashariki ya Kati bila suluhisho la “mataifa mawili,” na hivyo kutoa tahadhari wakati Saudi Arabia ikiwa na mpango wa kutambua utaifa wa Israeli.

"Wale wanaofikiri kuwa amani inaweza kutawala katika Mashariki ya Kati bila watu wa Palestina kufurahia haki zao kamili, na halali za kitaifa watakuwa wamekosea," Abbas aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kiongozi huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 87 alitoa wito mpya wa mazungumzo, na kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuitisha mkutano wa kimataifa kuhusu kuunda taifa la Palestina.

Marekani ina historia ya upatanishi wa amani kati ya pande hizo mbili, na Rais Joe Biden alizungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwenye Umoja wa Mataifa Jumatano, kuhusu kuhifadhi njia ya kufikia suluhu ya mataifa mawili.

Lakini serikali ya Netanyahu yenye misimamo mikali, ya mrengo wa kulia, imeendelea na ujenzi wa makazi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, unaochukuliwa kuwa kinyume cha sheria kimataifa.

Hotuba ya Abbas ilikuja siku moja baada ya Netanyahu kuzungumza kuhusu uwezekano wa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Saudi Arabia, wakati wa mkutano wake na Rais Biden.

Forum

XS
SM
MD
LG