Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 17, 2026 Local time: 12:19

Israel yavamia mji wa Palestina

Jeshi la Israel, Ijumaa limeuvamia mji wa Palestina kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, na kuzingira  jengo la makazi ya watu.

Tukio hilo limezusha ufyatuliwaji risasi baina ya kikundi cha wanamgambo cha eneo hilo ambao umesababisha kifo cha mwalimu mmoja ambaye hakuhusika na mapigano hayo familia yake na maafisa wa afya wa Palestina wamesema.

Ni shambulio la sasa kabisa kati ya mfululizo wa uvamizi wa jeshi katika himaya hiyo inayokaliwa kimabavu na kusababisha idadi kubwa ya vifo vya Wapalestina.

Vikosi vya usalama vya Israel vilivamia mji ulopo karibu na Tubas kaskazini mwa mji wa Palestina wa Nablus, na kuzunguka nyumba ambapo wanamgambo waliaminika kujificha.

Wanajeshi wa Israel waliwataka wanamgambo hao wanaotafutwa kujisalimisha kwa kutumia kipaza sauti kwa mujibu wa taarifa za wakazi wa eneo hilo.

This item is part of

Forum

XS
SM
MD
LG