Wakati akihudhuria sherehe za kuapishwa rais Mohamed Abdullahi Mohamed mjini Mogadishu Jumatano, Uhuru amewapongeza wananchi wa Somalia kwa kuendesha uchaguzi wa Februari 8 kwa amani.
“Wananchi wa Somalia wametoa kauli yao na wana matumaini makubwa juu ya serikali yao mpya katika kulijenga na kuliendeleza taifa hilo,” Rais Kenyatta amesema.
“Wewe Rais pia unachukua madaraka wakati tunakabiliwa na changamoto nyingi na tutaendelea kushirikiana katika kurejesha utulivu katika eneo la Pembe ya Afrika wakati tukikabiliana na ujangili wa kimataifa na mipakani.
Na ninaamini kuwa Mungu atakupa hekima ya kukabiliana na changamoto hizi,” Rais amesema.
Amezitaka jumuiya ya kimataifa na za kimaeneo kama vile IGAD na AU kusaidia Somalia katika maeneo muhimu.