Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:08

Kenya yawaondolea Washona msururu wa matatizo kwa kuwapa uraia


Jamii ya Washona Kenya walioishi bila uraia kwa zaidi ya miaka 50. (photo courtesy: Chief Joshua Kimemia)
Jamii ya Washona Kenya walioishi bila uraia kwa zaidi ya miaka 50. (photo courtesy: Chief Joshua Kimemia)

Mataifa yote barani Afrika yana makundi ya raia waliohama kutoka mataifa mengine.

Baadhi ya wahamiaji hao hukosa stakabadhi muhimu kama vile vyeti vya kuzaliwa na kukosa uwezo wa kuendeleza maisha yao ya kawaida. Nchini Kenya jamii ya Shona kutoka Zimbabwe imetambuliwa kama jamii moja ya Kenya na kuhitimisha msururu wa masaibu waliokuwa wakikumbana nayo kutokana na kutotambuliwa.

Washona waliwasili nchini Kenya kama Wamishionari kutoka Zimbabwe. Lakini hawakurejea kwao na badala yake wakaamua kuishi nchini. Wengi wao wanaishi katika maeneo ya Kinoo na Kiambaa katika Kaunti ya Kiambu ambako wanajishughulisha na kazi za mikono kama utengenezaji vikapu.

Hata hivyo maisha yao yalikumbwa na misukosuko mingi kwani si rahisi kuishi Kenya bila ya vyeti vya kuzaliwa na kitambulisho.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:33 0:00


Sasa mwito wao wa kuitaka serikali ya kenya kuwatambua ulitimia hivi karibuni walipokabidhiwa vyeti vya kutambuliwa ikiwa mwisho wa juhudi zao za miaka minne kutafuta vyeti hivi.

Baada ya mchakato huo uliohusisha mazungumzo na hata maandamano katika majengo ya bunge mwezi Oktoba pamoja na mjadala na viongozi wa Jimbo la Kiambu nchini Kenya, zaidi ya watu 2,000 kutoka jamii ya washoma wanaweza kutafuta stakabadhi muhimu za kitaifa kama wakenya wengine.

Rais Kenyatta aliyapa makundi hayo mawili vyeti vya uraia Jumamosi wakati wa sherehe za Sikukuu ya Jamhuri Dei katika uwanja wa Nyayo, Nairobi.

Imetayarishwa na Ubah Abdi kutoka Nairobi

XS
SM
MD
LG