Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 06:57

Kenya yafunga mpaka wake na Somalia


Watalii katika pwani ya mji wa Lamu nchini Kenya
Watalii katika pwani ya mji wa Lamu nchini Kenya

Wanajeshi wapelekwa eneo la mpakani na Somalia na serikali yasema huenda wakaingia ndani ya Somalia

Jeshi la Kenya limeamrishwa kuchukua hatua za kuzuia kundi la kigaidi la al-Shabab kuendelea na harakati zake za kuhatarisha usalama na uchumi wa Kenya. Hatua hiyo inakuja baada ya Kenya kutangaza kufunga mpaka wake na Somalia mwishoni mwa wiki.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jumamosi Waziri wa Usalama wa taifa Prof. George Saitori alisema Kenya inatangaza vita dhidi ya kundi hilo la kigaidi na kwamba majeshi ya Kenya yataingia hadi Somalia kuwasaka wanamgambo wa al-Shabab.

Vyombo vya habari Kenya vinaripoti kuwa msafara wa malori ya jeshi uliondoka Nanyuki kuelekea Moyale Jumamosi asubuhi, huku vikosi vingine vikiwa vinaelekea eneo la Wajir. Kuna ripoti pia kuwa jeshi la majini la Kenya lilishambulia boti mbili za spidi kali karibu na Lamu baada ya boti hizo kutotii amri ya kusimama.

Hatua hiyo inafuatia kutekwa kwa madaktari wawili wanawake mapema wiki hii kutoka kambi ya Daadab inayohifadhi wakimbizi wa njaa kutoka Somalia. Prof. Saitoti amesema wakimbizi wa Kisomali waliopo Daadab sasa watafanyiwa uchunguzi kwa sababu inaelekea kuna wafuasi wa al-Shabab miongoni mwa wakimbizi hao.

XS
SM
MD
LG