Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:18

Kenya: Waziri wa zamani wa elimu afariki


Waziri wa Elimu wa Kenya George Magoha akutana na wanafunzi wa shule iliyoporomoka mjini Nairobi Septemba 23 2019.
Waziri wa Elimu wa Kenya George Magoha akutana na wanafunzi wa shule iliyoporomoka mjini Nairobi Septemba 23 2019.

Waziri wa zamani wa elimu wa Kenya Profesa George Magoha amefariki. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na gazeti la Daily Nation, mke wake Dkt  Magoha amethibitisha kifo hicho.

Magoha amekufa wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali binafsi mjini Nairobi alikokimbizwa baada ya kupata matatizo ya moyo.

Profesa Magoha atakumbukwa kama waziri aliyekuwa na uadilifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yake kwenye wizara hiyo. Atakumbukwa pia kwa kuwepo ofisini wakati wa mtaala mpya wa elimu wa CBC na pia alikuwa mstari wa mbele kupanga mikakati ya elimu katika kipindi kigumu cha janga la Covid-19.

Taarifa za kifo chake zimekuja siku chache tu baada ya chuo kikuu cha Maseno kutangaza kwamba angejiunga tena kama profesa wa kufundisha kwenye kitengo cha matibabu.

Kifo chake ni pigo kubwa kwa familia yake kwasababu ndugu yake Profesa Richard Nyabera Magoha alikuwa azikwe Jumamosi wiki hii baada ya kufariki akiwa Marekani Desemba 6, 2022. Mwezi Agosti mwaka uliopita, Magoha alimpoteza ndugu yake mwingine Charles Agunga Magoha aliyefariki akiwa Sweden.

XS
SM
MD
LG