Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:26

Kenya: Odinga asema ataheshimu maamuzi ya mahakama


Bw. Raila Odinga
Bw. Raila Odinga

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye anapinga kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais wa mwezi huu kwenye  Mahakama ya Juu, amesema ataheshimu maamuzi ya mahakama – lakini bado anaamini alishinda.

Timu ya wanasheria ya Odinga imefungua kesi ikidai kuwa timu inayofanya kazi na Naibu Rais William Ruto ilidukua mfumo wa uchaguzi na kubadilisha picha halisi za fomu za matokeo ya vituo vya uchaguzi kwa zile zilizoghushiwa, hivyo kuongeza idadi ya kura za Ruto katika uchaguzi wa Agosti 9.

Ruto, ambaye alitangazwa rais mteule, amekanusha shutuma hizo. Tume ya uchaguzi imegawanyika na kuwasilisha majibu yenye kukinzana – makamishna wanne wamekataa kuyatambua matokeo, na mwenyekiti na wengine wawili wamekubaliana na matokeo.

Jopo la Majaji Maarufu wa Afrika limewasili nchini Kenya kufuatilia kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Urais Kenya 2022, ambapo kongamano linafanyika kabla ya kesi kuanza kusikilizwa Jumanne.

Kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na mgombea urais Raila Odinga, kati ya wagombea wanane wengine, anapinga matokeo ya upigaji kura wa Agosti 9 ambapo Makamu Rais William Ruto alitangazwa Rais mteule kwa kupata asilima 50.49 ya kura.

Dkt Ruto alitangazwa mshindi huku makamishna wanne wa tume ya uchaguzi IEBC, walimshutumu mwenyekiti Wafula Chebukati kwa kuuteka mchakato huo na kufanya maamuzi ya kumtangaza mshindi peke yake.

Jopo la wanachama wa Safu ya Majaji wa Afrika (AJJF) linaongozwa na Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.

Majaji wengine ni Lillian Tibatemwa -Ekirikubinza wa Mahakama ya Juu ya Uganda, Ivy Kamanga kutoka Mahakama ya Juu ya Rufaa ya Malawi, Moses Chinhengo kutoka Mahakama ya Rufaa, Lesotho, na Henry Boissie Mbha, Rais wa Mahakama ya Uchaguzi ya Afrika Kusini.

XS
SM
MD
LG