Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 23:12

Kenya na Haiti zasaini makubaliano ya kuwapeleka polisi Haiti


Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry,(L) akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje Dkt. Abraham Korir Sing'Oei huko Nairobi Machi 1, 2024. Picha na SIMON MAINA / AFP
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry,(L) akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje Dkt. Abraham Korir Sing'Oei huko Nairobi Machi 1, 2024. Picha na SIMON MAINA / AFP

Kenya na Haiti siku ya Ijumaa zimetia saini makubaliano ya pande mbili ya kupeleka polisi kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki, kuongoza kikosi kinachoungwa mkono na UN ili kupambana na magenge ya uhalifu nchini Haiti, amesema William Ruto.

Ruto amesema yeye na waziri mkuu wa Haiti Ariel Henry walijadili hatua zinazofuata kwa ajili ya kuwezesha upelekaji wa haraka, lakini haikuwa wazi mara moja kama makubaliano hayo yataingilia maamuzi ya mahakama yaliyotolewa mwezi Januari yaliyosema kwamba hatua ya kupeleka polisi Haiti ni kinyume cha sheria.

Kenya awali ilisema kwamba ilikuwa tayari kupeleka maafisa wa polisi 1,000 hatua ambayo ilipokelewa vyema na Marekani na mataifa mengine ambayo yalifuta uwezekano wa kupeleka vikosi vyake huko.

Lakini mahakama ya Nairobi ilisema kuwa uamuzi huo ulikuwa kinyume cha katiba kwa sehemu kwa sababu nchi hizo hazijatia saini makubaliano ya pande mbili kuhusiana na suala hilo.

Leo Ruto amesema yeye na Henry wameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya pande mbili katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kupelekwa ujumbe huo mwezi Oktoba mwaka jana lakini wasiwasi nchini Kenya kuhusu polisi hao kuhusika ulipelekea maamuzi hayo ya mahakama.

Forum

XS
SM
MD
LG