Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:53

Canada yatoa msaada wa dola milioni 60 kwa mpango wa kupeleka maafisa Haiti


Ghasia za magenge ya uhalifu Haiti
Ghasia za magenge ya uhalifu Haiti

Canada Alhamisi ilitangaza msaada wa dola  milioni 91 za Marekani kwa Haiti, ikiwa ni pamoja na takriban dola milioni 60 kwa ajili ya kutumwa kwa ujumbe wa kimataifa unaoongozwa na Kenya kusaidia polisi wa Haiti kupambana na magenge ya wahalifu.

Hayo yanajiri wakati taifa hilo la Karibean likikabiliwa na janga la kibinadamu.

Usaidizi wa Kanada "utachangia kufungua njia ya uingiliaji kati wa maana zaidi kulinda watu wa Haiti na kuhimiza juhudi zinazoongozwa na Haiti kurejesha amani na ustawi nchini," Waziri wa Mambo ya Nje Melanie Joly alisema katika taarifa.

Magenge yamekua yakiongezeka tangu vurugu kuzuka nchini Haiti hapo mwaka 2021 kufuatia kuuawa kwa aliyekuwa Rais kwa wakati huo Jovenel Moise.

Vita vilivyotokana na mauaji hayo vimefanya serikali kupoteza udhibiti wa baadhi ya maeneo nchini humo na makabaliano kati ya polisi na magenge kuongezeka.

Februari mwaka huu, serikali ya Canada ilituma ndege ya kijeshi kupaa juu ya Haiti ili kusuluhisha kile ilichoita hali tete ya usalama na kutatiza shughuli za magenge ya Haiti.

Mahakama moja ya Kenya iliamuru hivi karibunmi kwamba hatua ya kuwapeleka maafisa nchini Haiti ni kinyume cha katiba. Hata hivyo, Utawala wa Rais William Ruto ulisema ungekata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Forum

XS
SM
MD
LG