Hatua hiyo ya Kenyatta, vyanzo vya habari vinasema, imekuja baada ya Dkt Ruto kumpigia simu bosi wake akitaka kujua kwa nini Murathe anaendelea kushikilia wadhifa wake hata baada ya kutoa maoni yanayo kusudia kuisambaratisha Jubilee.”
Akionekana kama ni sauti ya Rais Kenyatta na asiye weza kubadilisha msimamo wake, Murathe Jumamosi alianzisha tena juhudi zake dhidi ya Ruto akiwa na nia ya kuingia Ikulu 2022, akisisitiza kuwa Ruto tayari aligombea kwa ticketi ya pamoja na Rais mwaka 2013 na 2017 na hivyo aache kugombea tena mwaka 2022.
Maoni hayo mara moja yalipingwa na wafuasi wa Dkt Ruto katika eneo la Rift Valley, na baadhi ya wabunge wakimtaka Kenyatta kumdhibiti Murathe “la sivyo Rais ajiuzulu na ajiunge na Raila Odinga katika upinzani.”
Kadhalika kulikuwa na wasiwasi, kufuatia tukio lililo nadra, la mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa bila kusita na Mbunge Kimani Ngunjiri, ambapo alimlaumu Rais waziwazi kwa kuleta mpasuko ndani ya Jubilee.