Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 28, 2023 Local time: 07:04

KENYA: Mbunge ahukumiwa miaka 67 gerezani kwa ufisadi


Mwanaharakati wa kupinga ufisadi katika maandamano nje ya bunge la Kenya. May 31 2018. PICHA: AP

Mahakama kuu nchini Kenya imemhukumu mbunge miaka 67 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya ufisadi.

John Waluke (57), mbunge wa Sirisia, Kaunti ya Bungoma, magharibi mwa Kenya, amepatikana na makosa ya kulaghai bodi ya kitaifa ya nafaka, kiasi cha shilingi milioni 313.

Alikuwa ameachiliwa kwa dhamana baada ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya chini.

Akitoa uamuzi wake, jaji wa mahakama kuu Esther Maina, amesema kwamba “mashtaka dhidi ya Waluhe na mwenzake Grace Wakhungu, yaliyokuwa yakisikilizwa na jaji Elizabeth Juma, yana Ushahidi wa kutosha dhidi ya washitakiwa. Huku waliyopewa sio kali zaidi ya inavyostahili. Ni hukumu iliyo katika sheria na hivyo kuhumu hiyo imekubaliwa na Mahakama hii.”

Mbunge Waluke alihukumiwa miaka 67 gerezani, huku mwenzake Grace Wakhungu akihukumiwa miaka 69.

Wakhungu ni dada wa aliyekuwa makam wa rais wa Kenya Moody Awori. Ni mama wa aliyekuwa waziri wa mazingira nchini Kenya, Judy Wakhungu.

Mbunge Waluke alikuwa amepewa nafasi ya kulipa faini ya shilingi milioni 727 huku Wakhungu akitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 707 lakini wawili hao waliamua kukata rufaa.

Waluke aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 huku Wakhungu akiachiliwa kwa dhama ya shilingi milioni 20 pesa taslim, Septemba mwaka 2020, baada ya kukaa gerezani kwa mda wa miezi 3.

Mahakama kuu imewapa nafasi nyingine ya kukataa rufaa ndani ya siku 14, la sivyo watumikie kifungo cha miaka 67 na 69 mtawalia.

Makosa dhidi yao

Waluke na Wakhungu walizuiliwa gerezani June 22, 2020 katika mahakama ya kusikiliza kesi za ufisadi, baada ya kupatikana na makosa ya ulaghai na kupokea kiasi cha shilingi milioni 297 kwa njia za ujanja, kutoka kwa bodi ya kitaifa ya nafaka NCPB, mwaka 2013.

“Nyaraka za madai ya malipo zilizotumika kutoa pesa hizo zilikuwa ghushi. Walike aliwasilisha nyaraka hizo akiwa anajua vyema kwamba hazikuwa halali,” amesema jaji Maina.

Wawili hao wanakabiliwa na mashtaka 5 yanayohusiana na kughushi stakabadhi za malipo, kutoa Ushahidi wa uongo na kujipatia mali ya uma kwa njia za ujanja, makosa ambayo walifanya kati ya mwaka 2009 na 2013.

Wasimamizi wa mashtaka walikuwa na mashahidi 27 katika kesi hiyo ya ufisadi iliyoanza baada ya kuchunguzwa na kamati ya bunge kuhusu matumizi ya pesa za uma.

Sakata ya kuagiza mahindi

Waluke na Wakhungu wanamiliki kampuni ya Erad.

July 2004, Kenya ilikabiliwa na uhaba mkubwa wa mahindi, na kupelekea kupanda kwa unga wa mahindi ambao unatumika sana nchini humo kama chakula cha kila siku kwa kutengeneza ugali.

Serikali ilitoa maelezo kwa bodi ya nafaka nchini Kenya- NCPB, kuagiza mahindi kutoka nje ya nchi ili kutosheleza mahitaji ya nchi.

NCPB ilitangaza zabuni ya tani 180,000 za mahindi.

Kampuni ya Erad, yake Waluke na Wakhugu, ilipata zabuni za kuagiza tani 40,000 za mahindi lakini haikupewa barua rasmi. Kampuni zingine nne zilizopata zabuni hiyo zilipewa barua rasmi.

Nne hizo ni Hala General Trading LLC ambayo ilipewa zabuni ya tani 40,000

Versatrade international iliyopewa tani 40,000

Purma Holdings, tani 30,000

Freba Investments, tani 30,000

Kesi mahakamani

Kulingana na waendesha mashtaka, Erad, ambayo ni kampuni ya Waluke na Wakhungu, haikuagiza mahindi licha ya kupata tenda.

Waluke na Wakhungu wanadai malipo pasipo kuagiza mahindi

Mda wa kuagiza na kuasilisha mahindi ulipokamilika, kampuni yake Waluke na Wakhungu iliwasilisha malalamishi kwa bodi ya nafaka ikitaka fidia kwa kukosa kupewa stakabadhi muhimu ambazo zingeiwezesha kuagisa mahindi kwa sababu ilipata zabuni ya kufanya hivyo lakini zabuni hiyo haikuwekwa rasmi na wahusika.

Waendesha mashataka badala yake waliasilisha kesi mahakamani kwa msingi kwamba stakabadhi walizoasilsha Waluke na Wakhungu zilikuwa feki na hivyo kesi hiyo ilikuwa ulaghai mtupu.

Mawakili wa kampini yake Waluke, walidai kwamba bodi ya nafaka ilikiuka mkataba kati yake na kampui ya Erad.

Erad ilipewa fidia kwa msingi kwamba mkataba ulivunjwa. Ilipewa dola milioni 1,960,000 kwa kupoteza faida, na dola 1,146,000 kama gharama ya sehemu ambayo walikuwa wametenga kuweka mahindi baada ya kuagiza.

Namna kesi dhidi ya Waluke na Wakhungu inavyoendelea

 • July 2004 - Uhaba mkubwa wa mahindi unatokea Kenya. Bodi ya kitaifa ya nafaka NCPB, inatangaza zabuni ya kuagiza tani 189,000 za mahindi kutoka nje ya nchi. Kampuni ya Erad ya Waluke na Wakhungu inakuwa mojawapo ya kampuni zilizoshinda zabuni.
 • Agosti 12 2004 – NCPB inatoa barua ya kuidhinisha kampuni ya Erad kuagiza tani 40,000 za mahindi kwa gharama yad ola 229 kila tani.
 • Agosti 26 2004 – Makubaliano kati ya Erad na NCPB yanasainiwa. Erad inapewa mda wa mwezi mmoja kuhakikisha kwamba mahindi yanaingia Kenya. Mda huo unaanza Agosti 26 2004
 • July 7 2009 – Kesi ya usuluhishi inaanza kusikilizwa baada ya kampuni ya Erad kudai gharama ya kuhifadhi mahidni ya asilimia 12.
 • Oktoba 6 2009 - NCPB inawasilisha kesi katika mahakama kuu kupinga maombi ya Erad.
 • June 28 2011 – Mahakama kuu yafutilia mbali kesi ya NCPB iliyopinga kutolewa malipo kwa Erad.
 • July 4 2011 – NCPB inatuma maombi kwa mahakama kukata rufaa
 • Januari 27 2012 – NCPB inakata rufaa namba 9/2012
 • Desemba 18 2012 – maombi ya NCPB yakataliwa na mahakama ya rufaa.
 • Septemba 2012 – Kampuni ya Erad yaishitaki bodi ya nafaka
 • Februari 27 2013 – Mahakama yaamuru NCPB kulipa Erad milioni 297,386,505
 • Novemba 20 2013 – Kamati ya bunge kuhusu matumizi ya pesa za uma inaanza uchunguzi kuhusu namna malipo yalivyotolewa na Sakata nzima ya uagizaji wa mahindi.
 • July 11 2014 – Mahakama ya rufaa inatupilia mbali jaribio la NCPB la kutaka kuasilisha ripoti ya bunge kama Ushahidi katika hatua ya kukata rufaa uamuzi wa mahakama hiyo. Mahakama ya rufaa ilisema kwamba Ushahidi uliokuwa unawasilishwa haukuwa umewasilishwa katika mahakama kuu.
 • Novemba 6 2014 – Tume ya kupambana na ufisadi EACC, inaomba kuwa sehemu ya kesi hiyo.
 • Desemba 18 2014 – Mahakama ya rufaa inakubali ombi la EACC kwa msingi kwamba kesi hiyo ilikuwa inahusu ufisadi na tume hiyo ndiyo yenye mamlaka ya kuchunguza ufisadi nchini Kenya.
 • Agosti 2 2018 – kampuni ya Waluke na Wakhungu (Erad) inafunguliwa mashtaka ya kughushi stakabadhi za malipo ya kiasi cha dola 1,146,000 kama Ushahidi katika kesi dhidi ya NCPB.
 • Januari 18 2019 – Washitakiwa wapinga kesi iliyokuwa ikiendelea kwamba ilikuwa imeanzishwa kwa misingi ya ripoti ya bunge ambayo iliandikwa wakati swala hilo lilikuwa mahakamani, na kwamba bunge liliingia kazi ya mahakama.
 • June 2020 - Walukhe na Wakhungu wapatikana na makosa ya kulaghai bodi ya kitaifa ya nafaka, shilingi milioni 297, na kuachiliwa kwa dhama miezi 3 baadaye.

XS
SM
MD
LG