Basi tuanze na usemi muhimu juu ya baba. Mafanikio yana kinababa wengi lakini mambo yanayofeli ni sawa na yatima.
Yatima ni mtoto ambaye wazazi wake wawili wamekufa. Bila ya wazazi, yatima bila shaka mara nyingi hujihisi mpweke duniani. Hakuna mtu ambaye anajitokeza kuwasimamia, tuseme hilo.
Hivyo hivyo tunaweza kusema juu ya mambo yasiyo na mafanikio. Mara nyingi watu hawatataka kabisa kujinasibisha na mambo yaliokuwa hayana mafanikio.
Watu huenda wasitake kuchukua jukumu, kwa mfano, katika mradi wa ofisini ambao hauna mafanikio – wewe unajua, mradi huo umefeli.
Kwa upande mwengine sio jambo lisilo la kawaida kwa watu kupigania kumiliki jambo lenye mafanikio. Siku zote wanataka wawe upande sahihi wa historia.
Utasikia wanasema : “Hilo lilikuwa wazo langu!” “Hapana, halikuwa wazo langu. Nilikuwa nalifikiria miaka mingi iliopita.” “Sawa, nilifanya takriban sehemu kubwa ya kazi hiyo.”
Hivyo basi unapata picha.
Kwa hiyo, msemo huu unamaana kuwa watu wanapenda kushiriki katika njia ya mafanikio na kujitenga mbali na jambo lililofeli.
Hivi ndivyo unavyoweza kutumia usemi huu.
Tuseme biashara mpya inaanzishwa katika jamii yako. Kila mtu anashauku juu ya hilo! Baadhi ya watu watawekeza fedha zao. Inakuwa ni gumzo mjini. Halafu, mara biashara inafeli. Watu ambao mwanzoni walikuwa wanaunga mkono wanaonekana kutokumbuka tena kuwa walikuwa wanaiunga mkono biashara hiyo.
Wakati watu hao wakikwambia, “Nilikuwa najua kuwa itafeli. Ilikuwa inaonyesha kutofanikiwa tangia mwanzoni.” Unaweza kuwaambia, “ Mafanikio yana baba wengi lakini kufeli ni sawa na mtoto yatima.”
Na sasa unaweza kusema kufikia kuliunganisha taifa la Marekani ni mafanikio. Na kuna kundi la wanaume ambao wanajulikana kwamba walikuwa upande sahihi wa historia.
Sisi tunawaita Founding Fathers, waasisi wa taifa hili.
Tunaweka herufi kubwa katika maneno haya mawili Founding Fathers tunapokuwa tunamzungumzia mtu yoyote aliye shiriki kuandika Katiba ya Marekani 1787. Baadhi ya Waasisi wa taifa hili maarufu kuliko wote ni George Washington, Thomas Jefferson, John Adams na Benjamin Franklin.