Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 18:02

Katibu mkuu wa UN aishutumu Russia kuyumbisha dunia


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akipeana mkono na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy katika mji Kyiv, Ukraine Machi 8, 2023. Picha na shirika la habari la REUTERS/Alina Yarysh.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumatano alishutumu uvamizi wa Russia nchini Ukraine uliodumu kwa kipindi cha mwaka mmoja kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Guterres alisema hayo alipowasili katika mjini Kyiv kwa mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kuhusu kuongeza muda wa usafirishaji wa shehena ya nafaka kutoka nchi hiyo iliyokumbwa na vita na uhakikisho wa usalama wa huko Zaporizhia.

"Haki ya kujitawala, uhuru, umoja na uadilifu wa Ukraine lazima idumishwe, ndani ya mipaka yake inayotambuliwa kimataifa," Guterres alisema kabla ya mazungumzo na Zelenskyy.

"Lengo letu kuu liko wazi: ni amani na haki kulingana na mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria ya kimataifa na azimio la hivi karibuni la baraza kuu kuadhimisha mwaka mmoja tangu vita ianze," alisema.

Lakini huku mapigano yakiendelea na hakuna mazungumzo ya amani yanayotarajiwa Guterres alisema Umoja wa Mataifa unajaribu "kupunguza athari za mzozo huo, ambao umesababisha mateso makubwa kwa watu wa Ukraine - pamoja na athari kubwa ulimwenguni."

Alitaka kuendelezwa kwa usafirishaji wa nafaka za Ukraine kupitia bahari ya Black Sea kwa ridhaa ya Russia. Alisema tangu mwezi Julai mwaka jana, tani milioni 23 za nafaka zimesafirishwa kutoka bandari za Ukraine, kiwango kikubwa cha nafaka hizo kilisafirishwa kuelekea nchi maskini. Lakini bila kuwa na makubaliano mapya mpango huo unatakiwa kumalizika tarehe 18 mwezi Machi .

Guterres alisema usafirishaji wa nafaka “umechangia kupunguza gharama za chakula duniani na umetoa unafuu mkubwa kwa watu, ambao vita vimewaathiri kwa kiwango kikubwa, hususani katika nchi zinazoendelea.

Hakika, rekodi za shirika la chakula na kilimo zinaonyesha bei za vyakula zimeshuka kwa takriban asilimia 20 katika kipindi cha mwaka uliopita.

"Usafirishaji wa bidhaa za Ukraine -pamoja na zile za Russia -chakula na mbolea ni muhimu kwa usalama wa chakula na bei ya chakula duniani," alisema Guterres.

Pia alitoa wito wa "kuondolewa kwa kijeshi yote" kwenye eneo lililo jirani na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia, kinu kikubwa zaidi barani Ulaya, ambapo mapigano yanayotokea katika maeneo jirani na kinu hicho yamesababisha kufungwa mara kwa mara kwa mitambo ya kinu hicho na kuibua hofu ya madhara yatakayosababisha uharibifu wa kinu chicho cha nyuklia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG