Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 03:27

Kampuni ya Ujerumani yaanza utafiti kutathmini chanjo ya majaribio ya malaria


Chanjo ya malaria inalenga mbu wenye kuambukiza ugonjwa wa malaria.
Chanjo ya malaria inalenga mbu wenye kuambukiza ugonjwa wa malaria.

Kampuni ya Biotech ya Ujerumani Ijumaa imesema imeanza utafiti wa hatua ya awali ili kutathmini majaribio yake ya chanjo ya Malaria kwa binadamu.

Jaribio la kwanza linatarajiwa kuwaandikisha watu 60 wa kujitolea nchini Marekani ambao hawana historia ya Malaria kufanyiwa tathmini ya chanjo katika dozi tatu.

Hili ni jaribio la kwanza la mradi wa chanjo ya Malaria kutoka kampuni hiyo ya Biontech.

Juhudi hizi ni moja ya zile zinazolenga kushughulikia ugonjwa wa Malaria unaotokana na mbu ambao unasababisha vifo takriban watu laki sita kila mwaka , vifo vingi vikiwa ni vya watoto huko barani Afrika.

Muundo mgumu na mzunguko wa maisha ya vimelea vya malaria kwa muda mrefu umezuia juhudi za kutengenza chanjo.

Baada ya miongo kadhaa ya kazi , chanjo moja ya malaria iliidhinishwa, Mosquirix iliyotengenezwa na kampuni ya dawa ya Uingereza ya GSK, iliidhinishwa mwaka huu na shirika la Afya Duniani, lakini ukosefu wa ufadhili na uwezo wa biashara umezuia uwezo wa GSK kuzalisha dozi zaidi zinazohitajika.

XS
SM
MD
LG