Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:02

Malawi imeanza kutoa chanjo dhidi ya Malaria


Mtoto akipewa chanjo dhidi ya Malaria katika kijiji cha Tomali nchini Malawi
Mtoto akipewa chanjo dhidi ya Malaria katika kijiji cha Tomali nchini Malawi

Serikali ya Malawi kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO, wameanza kutoa chanjo dhidi ya Malaria kwa Watoto, ambayo imetajwa kuwa hatua kubwa sana katika kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo unaosababishwa na mbu.

Chanjo hiyo kwa jina RTSS, ilifanyiwa majaribio kwa zaidi ya Watoto milioni moja nchini Kenya, Ghana na Malawi na kuidhinishwa na shirika la afya duniani WHO.

Licha ya kwamba ufanisi wake ni asilimia 30 pekee, chanjo hiyo imeongeza matumaini ya kupunguza vifo kutokana na malaria.

Watu milioni 20 hugua Malaria kila mwaka nchini Malawi na 400,000 hufariki dunia kila mwaka. Kulingana na wizara ya afya ya Malawi, watu watano hufariki dunia nchini Malawi kila siku kutokana na Malaria, wengi wao wakiwa Watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 na akina mama waja wazito.

Watoto 330,000 watapewa chanjo hiyo katika awamu ya kwanza. Kila mtoto anahitaji dozi 4.

XS
SM
MD
LG