Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 20:05

Kagame aanza uongozi wa awamu ya tatu Rwanda


Rais Paul Kagame
Rais Paul Kagame

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, aameapishwa Ijumaa kuanza awamu yake ya tatu kama kiongozi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Sherehe ya kuapishwa kwa Kagame imefanyika katika uwanja wa kitaifa wa Amahoro, ulio katika mji mkuu wa Kigali.

Kagame ameapishwa na jaji mkuu wa nchi hiyo, Profesa Sam Rugege huku mkewe, Jeannette Kagame akisimama kando yake.

Wakati wa hafla hiyo, mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Rwanda, Patrick Namvumba, alimkabidhi Rais Kagame ngao na mkuki kama ishara ya ulinzi wa taifa.

Kwa mujibu wa katiba ya Rwanda, Kagame alitakiwa kula kiapo ndani ya siku 30 tangu matokeo ya uchaguzi wa urais kutangazwa rasmi.

Rwanda ilifanya uchaguzi tarehe nne mwezi huu ambapo Kagame alishinda kwa Zaidi ya asili mia 98 ya kura zilizopigwa.

Hafla hiyo imehuduriwa na marais na viongozi kadhaa wa serikali, wakiwemo Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Sudan, Omar Al Bashir.

XS
SM
MD
LG