Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:31

Juhudi za kukivunja Chama Tawala cha Ethiopia zakosolewa


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Uamuzi wa Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kukivunja chama tawala miezi kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020 umekosolewa na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali yake.

Katika mahojiano na VOA, Waziri wa Ulinzi Lemma Megerssa amesema hali ya kutokuwepo utulivu nchini inaonyesha siyo wakati muwafaka kuunda chama cha siasa kipya.

“Kuunganisha chama hiki siyo wakati muwafaka kwani kuna hatari nyingi. Tuko katika wakati wa mpito,” amesema. “Hatuna muda tena, siyo wakati wetu. Tunakabiliwa na matatizo kadhaa kutoka maeneo mbalimbali katika wakati huu finyu.”

Lemma hivi sasa anatembelea Marekani akiwa na ujumbe wake wanaokusudia kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi kati ya nchi hizi mbili.

Mwezi Novemba, Abiy alitangaza kuwa muungano wa vyama unaotawala nchini humo, EPRDF, utavunjwa na kuundwa chama kimoja kinachoitwa Prosperity Party.

Uamuzi huo umekuja baada ya wanachama wa muungano huo kupiga kura kuunga mkono mabadiliko hayo.

Mnamo Disemba 1, Waziri Mkuu alifanya sherehe katika mji mkuu kusheherekea kuzaliwa kwa chama kipya na kusema “Pia imeandaa programu iliyowazi na sheria ndogondogo na mpango wa miaka 10 utakaopeleka mafanikio ya Ethiopia,” vyombo vya habari vya taifa vimeripoti.

Lakini uamuzi huo umezua ukosoaji. Chama cha Tigrayan Peoples Liberation Front (TPLF) kimekataa kushiriki kupiga kura kuunda chama kipya.

Mwenyekiti wa TPLF na kaimu rais wa mkoa Debretsion Gebremichael amewaambia waandishi wa habari kwamba hatua hiyo “inadhoofisha mfumo wa muungano na inawanyang’anya wananchi uhuru wao wa kujitawala. Hatua hiyo ya kuunda muungano wa vyama haichatilia maanani hali iliyoko hivi sasa nchini.

XS
SM
MD
LG