Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 14:21

Juhudi za kidiplomasia zaendelea Kenya kurejesha amani DRC, huku vita ikiendelea


Rais Félix Tshisekedi (D) akipongezwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya nchi yake kusaini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Nairobi, Kenya, Aprili 8 2022.
Rais Félix Tshisekedi (D) akipongezwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya nchi yake kusaini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Nairobi, Kenya, Aprili 8 2022.

Mapigano yanaendelea Rutshuru nchini DRC kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali karibu na Mpaka wa Uganda na DRC pembeni ya mbuga ya wanyamapori ya Virunga. 

Mapigano yanaendelea Rutshuru nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali karibu na Mpaka wa Uganda na DRC pembeni ya mbuga ya wanyamapori ya Virunga.

Jeshi la Congo linajibu mashambulizi ya waasi hao ambao wameweka kambi zao kwenye milima ya Chazu na Runyonyi wilayani Rutshuru.

Mapigano hayo yameanza wakati ambapo serikali ya Congo imeanzisha mchakato wa kurejesha amani mashariki mwa nchi kwa kuzungumza na makundi ya waasi nchini Kenya Nairobi.

Wakati huo huo Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameyasihi makundi yenye silaha mashariki mwa DRC kuweka silaha zao chini na kufanya kazi na serikali katika kutafuta amani na uthabiti.

Wawakilishi wa makundi yenye silaha wanakutana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi kwa ajili ya mazungumzo moja kwa moja na maafisa wa DRC.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya maazimio yaliyopitishwa katika mkutano wa wakuu wa nchi za afrika mashariki . makundi ambayo hayatashiriki katika mazungumzo hayo yatashughulikiwa kijeshi , taarifa kutoka kwenye mkutano huo zimeeleza.

Rais Kenyatta amesisitiza kwamba bila kufanya kazi kwa umoja na ushirikiano miongoni mwa watu wa DRC, kila upande utakaobaki utakuwa umeshindwa.

Wawakilishi wa karibu makundi 30 yenye silaha wameshiriki katika mazungumzo hayo na wengi walikubali ombi la wakuu wawili wa nchi kuweka silaha chini wakati wengine wachache waliomba kupatiwa muda zaidi kujipanga na kuweka masharti lakini walionyesha utayari kuungana pamoja kujenga nchi,.

XS
SM
MD
LG