Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 01:32

Je, upo mfarakano kati ya Kenyatta na Ruto?


Rais Kenyatta (kulia) na Makamu wake Ruto

Kutoonekana Ikulu kwa Makamu wa Rais William Ruto bila kutolewa maelezo yoyote wakati Rais Uhuru Kenyatta akizindua sehemu ya kwanza ya baraza la mawaziri kumezua hisia na mazungumzo tofauti nchini Kenya.

Kumekuwa na dhana kwamba hilo siyo jambo la kawaida baina ya wadadasi wa kisiasa nchini Kenya na kwamba huenda upo mvutano kati ya viongozi hao ambao unaweza kutengeneza taswira mpya katika awamu ya pili ya utawala wao.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vimesema kuwa wasaidizi wa Ruto walithibitisha kuwa alikuwepo nchini wakati zoezi hilo la kutangaza baadhi ya mawaziri likiendelea, na pia alikwenda kazini katika ofisi yake ya Harambee, uamuzi wake wa kutojumuika na Rais Kenyatta wakati akizindua baadhi ya wateule wa baraza lake limeleta mshituko mkubwa serikalini na kila moja akijaribu kutabiri ni hatua ipi itakayofuatia.

Hata hivyo Ruto amezungumza juu ya uteuzi huo katika mitandao ya kijamii Jumapili na kukanusha kuwepo tofauti kati yake na Rais, akiwataka hasa wana jubilee kujiepusha na "malumbano ya kisiasa yasiokuwa na faida" juu ya uteuzi wa mawaziri.

Ametaka Rais aachiwe kutekeleza madaraka ya kikatiba ya kuchaguwa timu yake itakayo mwezesha kutekeleza ahadi za kampeni ya chama chake cha Jubilee.

Hitilafu ambayo inazungumziwa ni kuwa Ruto inasemekana kuwa hakubaliani na baadhi ya wateule wa Kenyatta ambao anataka kuwaleta katika baraza lake la mawaziri wakati atapotoa majina kamili ya baraza hilo.

Kadhalika inawezekana kwa sehemu kubwa kwamba Ruto aliamua kutohudhuria kuzinduliwa huko kama ni njia ya kuonyesha kutokubaliana naye bosi wake.

Chanzo cha habari ambacho kinafahamu mazungumzo yanayojiri katika uteuzi wa wale wanaotarajiwa kuwa mawaziri amesema kuwa makamu wa rais anaamini kuwa baadhi ya mawaziri ambao tayari wametemwa kutoka katika baraza hilo jipya na Rais walistahili kurudi katika baraza hilo, limeripoti gazeti la The Daily Nation la Kenya.

Wadadisi hao wanasema kuna hali mbili pengine Ruto amechelewa kupeleka pendekezo lake au baadhi ya majina anayotaka kupendekeza katika baraza hilo yamekataliwa.

Chanzo hicho cha habari kimesema kuwa Ruto mara ya mwisho alikuwa Ikulu Disemba 23 wakati yeye na Kenyatta walipokuwa katika mkutano ambao uliendelea mpaka usiku.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG